Habari

Wazanzibar tujipange kuwatetea Masheikh wa UAMSHO

Na Chatumpevu

Ijumaa Kareem kwenu nyote wazalanedo

Ninaposoma makala inayohusu UAMSHO huwa naumia sana. Hakuna asiyejua kuwa Masheikh hawa wamewekwa ndani kwa sababu ya dhulma na sio kuwa wamehusika na ugaidi. Haingii akilini miaka 5 ipite bila ya kupata ushahidi unaotafutwa na serikali badala yake serikali inawashikilia masheikh hawa wasio na hatia kwa sababu ya uislamu wao, uzanzibari wao na kusema kwao ukweli juu ya namna muungano unavyoendeshwa bila ya kuzingatia minzania ya usawa.

Serikali isidanganye umma, haichukui jitihada yoyote ya kutafuta ushahidi na viongozi wakubwa wamesikika wakisema kuwa waache ‘UAMSHO wafe jela’. Hakuna dhamira ya kisiasa ya kuwatoa masheikh hawa maskini na wasio na hatia. Cha ajabu ni kuwa kukamatwa, kutesewa ( wakati wa interrogation – mahojiano) na kukandamizwa kwa haki zao hakuna jumuiya hata moja ya haki za binadamu iliyowahi kukukemea uovu huu. Dunia imekaa kimya, human rights organisations za Tz zimekaa kimya, waislamu wa znz tumekaa kimya, ni kimya kikubwa na kizito kama kimya cha kaburini na hakuna efforts zozote zinazoendelea za uchechemuzi( activism ) za anagalau kupaza sauti ili wakubwa wasikie na wafahamu kuwa kinachondelea juu ya masheikh hawa sio haki. Ndiyo, yawezekana pengine tumetishwa juu ya namna ya kulishughulikia tatizo hili kama wananchi na wazanzibari na husuan pale walipokamatwa viongozi wa jumuiya maimamu walipokuwa wakiendesha michango ya kusaidia familia za masheikh wetu. Ndiyo, pengine awamu hii imekuwa ni ya kitisho zaidi na hususan pale mkuu wa kaya na mkoloni alipowahi kusema kuwa masheikh wa UAMSHO walihusika ktk kuistabalise Rufiji/ mkuranga kama mnakumbuka, tuhuma ambazo hazikuwa na mashiko na ushahidi. Ndiyo, pengine watawala wa znz wamewapeleka masheikh wetu kwa mkoloni makusudi ili kuwaogopesha waliobakia , hususan masheikh ambao wana uthubutu wa kusema lile lililo sahihi kusema ktk dini na siasa. Lakn ifike wakati mkoloni na vibaraka wake waseme kuwa wale UAMSHO ni binadamu na wanahaki zao.

Mbaya ziadi ni kuwa hata kati yetu wazanzibari tunatiliana fitina unapolizungumza suala hili la UAMSHO. Unaonekana kama vile na wewe ni sehemu ya kundi hilo lilio baya katk macho ya watawala. Kuna siku nilikuwa nililizungumza suala hili na baadhi ya marafiki zangu ,’ mmoja wao akasema’ waache yawakute wameyataka wenyewe’. Na huyu ni mzanzibari muislamu na wala hana asili ya kutoka kwa mkoloni lakn kwa sababu kapewa cheo ndo maana anapata jeuri ya kusema alivyosema.

Ukimya wetu utaendelea mpaka lini? Vuvuzela/ uchechemuzi una nafasi ktk advocacy alimradi unatumia njia ambazo hazitokuwa confrontational, njia za busara, njia za kistaarabu zitakazofanya IQ za wakubwa kuamka na kuwafanya watafakari, wajifunze, wachukue hatua na hatimaye kuwaachia masheikh wetu wa UAMSHO. Silence until when, forever? for whom? Hapana. Wallah machozi yananitoka ninapoandika makala hii nikikumbuka tabu na madhila waliyopatiwa waumini hawa wa kiislamu, mateso tosha ya kutenganishwa na familia zao , wake zao, watoto wao, wapendwa wao kwa miaka mitano sasa bila ya sababu yoyote , wallah haikubaliki na haikuji kabisa ktk ustaarabu wa binadamu.

Lkn kinachoendelea ni taswira yenye kiza kinene kisicho na hata dalili ya mwanga. Hali ni ngumu zaidi ktk awamu hii ya tano kwani ‘attitude’ ya mkuu wa kaya ni ya ukatili zaidi na hususan pale uislamu unapojionesha ktk uhalisia wake.

Nje ya pazia unaweza ukaona kuwa kushikiliwa kwa masheikh wetu ni kama vile Tanzania tunaidanganya dunia kuwa na wao wamo ktk vita dhidi ya ugaidi ili waendelee kupata misaada ya kimataifa. Lkn jee danganya toto ktk diplomasia ya kimataifa na ‘geopolitics’ itathibitisha madai haya ya ugaidi ktk Tz? Kuna wakati waziri wa mambo ya ndani aliyekuwa ( Mwigulu Mchemba ) aliwahi kusema kuwa Tz hakuna ugaidi, sasa iweje leo wahanga hawa wa Umsho waendelee kushikiliwa bila ya sababu? Ujue kuna jambo na jambo hili ni utashi tu wa kisiasa wa kuwafanya watawala waendelee kushika hatamu bila ya bughudha , na kwa kuwa masheikh waligusa dudu baya la kukosoa muungano ndo maana wamekuwa ni scapegoat (mbuzi wa kafara ) ktk taswira nzima ya kutafuta haki ya wazanzibari ktk muungano.

Niishie porojo zangu kwa kusema kuwa :

1. Tuvunje ukimya ktk kuwatetea wenzetu hawa
2. Tusiogope kusema
3. Tutumie kalamu zetu / keyboard zetu kusaidia ktk kupaza sauti za utetezi
4. Mimi na wewe tuwe na wajibu ktk harakati hizi.

Wasalam.

Share: