Habari

Wazanzibari Amkeni: Jini (CCM) Lishapanda Kichwani na sasa Lataka Damu zetu.

Asalamu aleikhum Warahmatullah Wabarakatun Ndugu zangu Wazanzibari na Watanganyika ambo munapenda kuiona Tanganyika na Zanzibar ina Democrasi ya kweli na utawala wa Haki sawa kwa pande zote mbili ambazo zimeunda muungano huu.

Ndugu zangu Wazanzibari, hakuna asiejuwa kwamba Balozi Sefu Ali Iddi aliwahi kusema kwamba mwisho wa CUF itakuwa ni 2015. Sababu yake kusema hivo nikwamba waliogopa kuja kupinduliwa kwa kukosa Majimbo yote ya Uwakilishi Unguja na Pemba. Hapo kulianza njama za kutayarishwa mgogoro ndani ya chama cha CUF ambao ulidumu kwa miaka 3½. Wengi wetu tulikuwa  tushachoka na kusikia timu ya maalimu wamefungua kesi na kesi hizo zikipigwa kalenda. Lakini pia tulijuwa kama CUF ya Wazanzibari ( sio ya Lipumba) ilikuwa ni Taasisi iliojengwa na ikawa ina wanachama Imara wasio yumbishwa wala kuwa na tamaa ya kununuliwa. Na rekodi za CUF ya Maalim kwa upande wa Zanzibar zinaonyesha kwamba kwa miaka 28 sasa yakuundwa CUF, hakuna hata kiongozi mwandamizi wa CUF au wanachama tulio wasikia wakihama CUF na kuhamia Vyama vyengine. Licha CCM kuwajaribu kutaka kuwanunua lakini walishindwa kwasababu iliokuwa CUF ya maalim Sefu ilikuwa na  Wanachama waliokuwa Wazalendo na walisimamia kile walichokiamini.

Sio hivo tu, mgogoro wa CUF uliopandikizwa wengi wetu tilikuwa hatujuwi kama Dola akiwemo Msajili walikuwa wakitumika. Na tulikuwa tunasikiliza malumbano ya Lipumba na CUF ya maalim kwa undani ili tupate ushahidi hasa na kiini cha mgogoro wao; Au kumjuwa  JINI MAPEMBE Alieletwa kuivuruga CUF, kweli ana Mkono wa CCM na Dola?

Naam jibu tumelipata siku ile ya tarehe 18.March 2019 wakati Maalim Sefu Sharif Hamad alipotangaza kuihama Chama  CUF,   ambae yeye na akina Ali Haji Pandu, Nassor Sefu  na vijana wengine wa Unguja na Pemba wakiwa na uchungu kukiacha Chama chao walichokuwa wakikipigania kwa nguvu na damu zao.

Baada ya tangazo hilo tuu  CUF-Lipumba ilianza kuweweseka na kupiga kelele, Jini likaja kichwani. Siku ya tarehe 20.March 2019 Jini likaanza kujitokeza kwa rangi zake za Kijani- katika mkutano uliofanywa na mmoja wa katika kundi la watu wasiojulikana; huyu mtu anaejiita DR. Bashiru sijuwi Bashuru, mimi namuona kijana huyu ni katika wapangaji wakumpiga Risasi Tundu Lissu. Dalili zote zinaonyesha watu wabaya wa CCM huwa hawawezi kujizuia na Siasa za Kistaarabu. Jini Hili limepanda kichwani kwa rangi zake na vitisho vya asili na lengo lake nikuwanyamazisha Wazanzibari ( ATI) nakuifuta ACT-Wazalendo.

Pale Komba wapya leo tumeshuhudia yule Kifaru mnene anaejiita Waziri wa Mambo ya Ndani akitoa Onyo kali kwa Wazanzibari hasa kule Pemba. Na kuagiza kwamba Polisi wawachukulie hatua viongozi ambao wamefanya mikutano.. Hivo tumuulize huyu Waziri wa Ndani, kifaru hichi cha mbugani. Nani yuko juu ya Sheria kama sio Nyinyi Mfumo dhalimu wa CCM?

Mwezi uliopita Polepole alifanya mkutano pamoja na Mwingulu Nchembe anakusanya watu akifanya mikutano ya hadhara. Wakati Magufuli amewafungia wapinzani wasikusanyike. Hii kweli ni haki?

Hivo hamujuwi kama Watanzania sio wajinga wala hawaogopi kutishwa?

Wiki mbili zilizopita Lipumba alifanya mkutano wakuchagua viongozi wapya wa Chama chake na polisi hao hao unaowataka Waende Pemba kupiga wananchi wanyonge ndio waliokuwa wamesimama kumlinda Lipumba mchana kweupe. Leo iwe kioja kwa Wazanzibari kukusanyika na kufurahi au kuoa matamko ya kidini imekuwa munawapelekea  UV-CCM ambao ndio hao watu wasiojulikana na munataka kuwa dhuru.

Sisi Wazanzibari tunasema enough its enough, mara hii wakija Vijana wa CCm kutukamatia watoto wetu hatutanyamaza. Polisi na Jeshi ni watu wanaoishi miataani na family zao tunazijuwa. Hivo ni bora CCm wakaangalia kauli zao za Mikutano na chuki wanazozifanya dhidi ya raia wasio na hatia.

Kama munataka kuipoteza amani ya nchi hii basi jitokezeni aktika Viunga vya Zanzibar na muanze kutukamatia watoto wetu, waume zetu au wake zetu. Na sisi tutawaonyesha. Vitisho vya Buldoza aliekuja jana na Bashiru sisi tunavichukulia kwamba Mumeshindwa katika jukwaa la Siasa na sasa munataka kutumia nguvu kama ilivo kawaida yenu.

 

Share: