Habari

Wazanzibari Tunasema: Hatuna haja ya Vyama, Tunataka Tupumue

Assalamu aleikhum warahmatullah wabarakatuhu ndugu Wazanzibari  na Watanganyika woote wa ndani na nje ya visiwa vyetu/ nchi yetu adhimu. Hakika bila yakupoteza muda napenda kujibu hoja, porojo na Speculation kubwa zinazo endelea hivi sasa kuhusiana na mambo haya 3 ambayo nimeona ndio yanazungumzwa sana na Social Media au wananchi.

1.Vyama vya Siasa (CUF).

2.Lipumba  na CCM.

3.Maali SEFU CHADEMA

 

Vyama vya Siasa (CUF):

Kama tunavoelewa kwamba vyama vya Siasa kwa upande wa visiwa vya Zanzibar vilikuwepo wakati wa miaka mingi sana ya ukoloni wa Wazungu. Na wakati huo nchi ya Tanganyika  ndio kwanza ilikuwa ina (Emarge) katika tope tope za umasikini, ukosefu wa elimu na maendeleo ya jamii au miundo mbinu. Vyama hivi  vya Siasa vilikuja Kuundwa tena wakati ule wakudai Uhuru na mfumo mwengine wa vyama vingi ulioanza 1989- Wakati wa kuanguka kwa Barlin Wall na Kuvunjika kwa USSR pamoja na tawala nyengine nyingi za Kidictorship. Nchi za Ulaya waliiangalia Africa na kuitathimini rasilimali zake na kutafakari kwamba licha yakuwa Nchi za KiAfrica ni Matajiri na wana rasilimali tofauti.  Lakini Uhuru  waliodai nakupatiwa kutoka kwa Mkoloni haukuweza kuwanufaisha Wananchi maskini na kunyanyuwa Uchumi wa Nchi hizo za Kiafrica kimaendeleo na kijamii.

Walizistajabia nchi hizi, kwanini baada ya miaka 50 ya Uhuru bado zinaendelea kuwa masikini na kuomba omba, na nyengine kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka nenda miaka rudi? Waliona wimbi la fedha za viongozi wa Kiafrica zikiwekwa katika Ma Bank ya Nje, kwavile hawawezi kusema hatutaki kuombwa ombwa – ndio maana wakaanzisha mfumo wa vyama vingi ili kutoa fursa kwa wananchi wa nchi zote walizokubali mfumo huu wa Kidemocrasia ya  siasa za vyama vingi, kuweza  kuikosoa Serikali ambayo haina faida na Wananchi wake;  kuwa na mtindo wa kubadilishana uongozi au kuunda Serikali za Umoja wa Vyama hivo-  pale chama kimoja au chengine kinaposhinda uchaguzi huru na wa haki. Na kuweza  kuongoza Nchi zao na kuleta maendeleo  ya kijamii na kuachana na Omba omba katika nchi za Ulaya au vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Hii ndio ajenda kubwa ya mfumo wa Vyama vingi na sio kuisifu Serikali na Viongozi tawala wanaofanya madudu;  kuwanunuwa  viongozi wa upinzani kwa pesa ya walipa kodi; au kuwauwa na kuwaweka mahabusi wale  wapinzani wanao jaribu kuikosowa Serikali au Mfumo mbovu uliopo madarakani.  Sio hivo tu, mfumo huu wa vyama vingi umezinufaisha Nchi nyingi  sana za Earsten European kama vile UK, Scandanevian, German, Holland, France nk. Na zile  Nchi zilizokuwa Masikini kule Wersten European kama vile Lartvia, Bosnia, Maccadonia, Kosovo, Lutherenia, George-  Au hata katika baadhi ya Nchi za Lartin American. Ambazo zimeanza  kuiga mfumo wa Kidemocrasia basi hivi sasa zinapiga hatuwa  za kiuchumi na kijamii. Mfano ni Brazil, Chile, Peru, Mexico, Cuba nk.

Tujiulize whats wrong with Africans, au watu wenye Ngizo Nyeusi? Kila anaekaa madarakani anataka Kunywa Damu za Raia wasiokuwa na hatia. Acha Wazungu wawe wanatutukana na kusema tunataka tuwe Re-Colonised… Wameona hakuna litakalo tufaa kwani akili zetu ni za tope.

Lakini kwa upande wetu wa Tanganyika na Zanzibar Nyerere alilipokea hili kama vile nikuwatia adabu Wazanzibari na kuendelea kutumia mfumo wa Chama kimoja Kushika hatamu hata kama itakuwa ni Kwa GOLI la MKONO. Tumeyaona miaka 25 ya Vyama vingi kwa upande wa Zanzibar CCm haijawahi kushinda Uchaguzi hata mmoja. lakini Wanatumia Magoli ya Mkono na kuwagombanisha Wazanzibari ili wapate kuendelea Kututawala Maisha. Ndugu wasomaji sitaki kuwarudisha katika historia ya Uhuru ila hapa nataka kuwavuta katika mwaka 1989-1992 wakati vyama hivi tulivonavo sasa vimekuwa tishio kubwa kwa utawala mbovu wa CCM uliokaa madarakani kwa miaka 57 sasa.  Na tuviangalie baadhi ya vyama vya akina Mtikila, Mrema, Hamadi Rashid au CUF ya Lipumba vilivo amua ku unyamazia utawala huu haramu wa CCM au kujiunga nao kufanya Uharamia huo kisiri siri.

Ndugu wasomaji siku ile 1992, Wazanzibari walipoambiwa kuna mfumo wa vyama vingi unaanza ndoto yao kubwa nikuanzisha chama chao wenyewe Wazanzibari “Nationalist Party” na Sio chama cha Muungano ambacho kitakuwa na wanachama kutoka Tanganyika na Zanzibar. Hii idea ya CUF, CCM, NCCR nk, kuwa na wanachama huku na huku ni mipango maalumu ya Nyerere  na serikali yake ya Tanganyika ambayo alitaka kuendelea kuidhibiti Zanzibar kwenye ukoloni  mambo leo (New Colonialisim) wa Tanganyika so call Koti la Muungano.

Wazanzibari walitaka kuwa na National party kwasababu ya kuchoshwa na uwongo, dharau, udhalima na ubadhirifu unaoendelea kufanywa na Serikali ya Tanganyika dhidi ya Zanzibar na Wazanzibari. Hivo basi  kwakutaka kuweka wazi kabisa sisi Wazanzibari hutushuhulishwi  tena na Vyama vya Siasa au kiongozi gani atapewa Ukatibu wa Vyama. Ikiwa CUF au CCM vitakufa leo basi Wazanzibari wako na msimamo ule ule wa kutaka Nchi yao au Visiwa vyao kuwa HURU. Na sio jengine.

LIPUMBA NA CCM:

Wazanzibari walimpokea Lipumba kama ndugu yao muislamu mwenzao na kumpa heshima na kumbeba katika nyoyo zao. Hili Lipumba hawezi kubisha. Lakini Lipumba aliebebwa na kuheshimiwa katika nyoyo za Wazanzibari ni yule Lipumba aliekuwa Muungwana na Mkweli sie huyu Lipumba MNAFIKI, MUONGO, MBAGUZI, MWIZI na MSAHAULIFU wa HAKI za Wazanzibari.

Lipumba ametufanyia dharau kubwa sana sisi Wazanzibari na hatuwezi kumsamehe- pale alipokuja Zanzibar kisiri siri na kuungana na Serikali HARAMU ya CCM iliowekwa madarakani 28.Octobr 2015 kwa Mtutu wa Bunduki na Jakaya Mrisho Kikwete. Sio hivo tuu Lipumba alisikilikana akisema kwamba CUF waingie kwenye Uchaguzi wa marudio wa 12.March 2016. Wakati akijuwa wazi Uchaguzi ule ulikuwa haramu na haukubaliki katika Katiba ya Zanzibar au hata hio katiba ya Tanganyika/ Muungano. Lipumba huyu huyu alijuwa Wazi kwamba Wazanzibari walichaguwa Chama cha Upinzani (CUF) ili kiweze kuiongoza Zanzibar kwa kipindi cha miaka 5. Na wakati huo tulikuwa na Serikali ya GNU ambayo ilikuwa ikiwakosesha Usingizi CCM na mfumo wao Kristo wa Utawala. Hivo hapa nikubadilisha Pillow Cover tu nakuachwa Wazanzibari wa Experiment uongozi wa CUF kama yalivokuwa malengo ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi.

Kama  Lipumba ni mpenzi wa CUF na Wazanzibari na anaipenda CUF na sio CCM; kwanini hakusimama na msimamo wa  Wazanzibari ambao walikuwa na Haki ya kuongozwa na Chama cha upinzani? Ikiwa Lipumba amethubutu pia kidharau Sheria na Katiba ya Zanzibar kweli huyu atakuwa na imani   na Wazanzibari wenyewe?Kama kweli yeye ni Mpezi wa Democrasia ya kweli na anaamini CUF na Umoja wa UKAWA aliouanzisha yeye kwanini hakukemea Mauwaji ya Waaandishi wa habari, kupigwa risasi kwa Lissu na matokeo mengine? Which Moral value & democracy  is he try to show Watanganyika and those who support him? Badala yake Lipumba huyu huyu anaendelea kuitumikia CCM ambayo ndio madhalimu wkubwa wa Zanzibar na Wazanzibari.  Tumeona udhalimu wao  waliokua wakiwafanyia Wazanzibari sasa hivi wanawafanyia Watanganyika wenzao tena Wakristo kama wao. Kweli CCM itakuwa na Imani na Muislamu Lipumba+. Hebu naajiulize yuko wapi Dr. Slaa? Mbona yeye hakupewa Cheo ktk Serikali ya Magufuli?.Kwanini Slaa apewe Cheo cha ubalozi? Ni nini hasa kikubwa ambacho DR Wilbrahim Slaa aliifanyia CCM hata apewe nafasi ya Ubalozi?  Nawasikitikia wale ndugu zetu wa Kizanzibari walioacha kazi nakutupa utu wao nakuungana na Lipumba.  Shame on them.. Hivo Kama LITUNGI atamkabidhi Lipumba CUF CC Wazanzibari hatujali na ampe Lipumba CUF aone kama atapata hata kura moja 2020.

MAALIM SEFU NA  CHADEMA:

Ndugu zangu Watanganyika ambo ni waumini wa Dini tofauti, nataka niwape siri moja kubwa ambayo tunayo sisi Nartive Zanzibari,  hasa wale watu wanaotoka katika Kisiwa Cha Pemba, Uzi na Tumbatu. Watu hawa wana Msimamo usio yumba kabisa ikiwa wanaamini kitu ambacho ni cha haki. Sisi Wazanzibari tunapokuwa tunaiona dalili ya Watu wanaotaka kutetea Haki ya kweli  nakuamini utawala wa Sheria na katiba bila yakuwa na dalili za kibaguzi ndani yake- basi huwa tuna ungana nao kimawazo na ki strategic ili tuwe na nguvu moja.  Sisi Wazanzibari hatuna ubaguzi wa  Rangi, Dini wala Kabila kama alivo Profesa Lipumba na akina Profesa Mtungi, Hando, Kata na Kufuli. Na ndio maana munamuona Maalim Sefu Sharif Hamadi  ameshikana na Chadema kutoka Day One 2014 wakati Lipumba alivoanzisha Umoja wa UKAWA ndani ya Bunge lao la Tanganyika. Maalim Sefu hakuweko Bungeni na alikuwa akitukanwa na CCM na Mamluki wengine ndani ya Bunge lile. Lakini alipoambiwa kwamba Lipumba na viongozi wa Upinzani  wametoka bungeni na wanakuja Zanzibar kwa wananchi. Wazanzibari woote walifurahi na kuwapokea kama watoto wao.

Kuna baadhi ya Viongozi wa Chadema walikuwa wakisema CUF ni chama cha KIISLAMU. Lakini tuliwasamehe na tukawapokea kwa Mikono na Miguu yetu. Na tumewaweka katika nyoyo zetu kama vile ni watu wa Dini moja, kabila moja au tumewazaa. Hii yote nikwasababu ya msimamo wao dhidi ya Udhalimu wa Serikali ya CCM.

Huyu Profesa Lipumba, Mtanganyika mwenzenu hakuweza kuyafanya  haya yakuwapokea Chadema kama Chama cha Upinzani na kuunganisha nguvu moja. Mifano tunayo na ni uchaguzi wa 2005-2010.  Yeye kama katibu Mkuu Taifa kwanini aliipigia kampeni CCM kwa wapiga kura wa Tanganyika ambao wako CUF?

Alianzisha ajenda ya Uislamu na Ukristo katika Uchaguzi wa 2005-2010 na hatimaye tunaona CCM ilikoifikisha Zanzibar na Wazanzibari na inakoipeleka Tanganyika na Uhuru wake. Miaka yote ya Mfumo wa Vyama Vingi CUF Tanganyika haijawahi hata mara moja kupata Viti vingi Bungeni. Na kwasababu huyu LIPUMBA ambae  kama ndie atakae kabidhiwa Chama cha CUF na Watanganyika wenzake Bara -ndie  huyu huyu aliekuwa akikiuwa Chama cha CUF kisifanye vizuri kwa Siasa zake za kibaguzi. Huo ndio mfano tosha wakuelewa kwamba Lipumba sio CUF ni CCM na Wale Wazanzibari au watanganyika wanaomuunga mkono Lipumba, akina Khalifa na Nassor Sefu wapo pale kwa faida ya matumbo yao  au wana chuki  zao binafsi na dhidi ya Viongozi wa CUF Zanzibar.

Ikiwa kutakuwa na Mtanganyika yoyote ambae bado anamuamini Lipumba kama ni CUF  basi naarudishe akili yake nyuma kidogo na ajiulize masuali haya.

Kama Kweli Chama cha CCM kinawapenda Waislamu wa Tanganyika ambao walimpa Jakaya Kikwete (CCM-Muislamu) kura zote ili amshinde Slaa (Chadema-Mkristo). Mbona Jakaya Kikwete alishindwa Kuwaletea Mahakama ya Kadhi? Nani ana tetea Waislamu Wapatiwe Mahakama ya Kadhi Tanganyika kama sio Chadema- Wakristo? Kwanini Gas ya Mtwara haiwanufaishi Wamakonde wa Mtwara ambao wengi ji Waislamu? Kwanini Dhahabu na Madini Mengine au rasilimali za Mali ya Asili zilioko Mikoa mengine ya Tanganyika zinawanufaisha Wananchi  mmoja mmoja wa Mikoa hiyo?

Hivo kwakumalizia point hii ndugu Watanganyika Waislamu acheni Ujinga wakumuamini Lipumba na CCM na Uislamu. CCM ni Chama cha Kikatili kama kile chama cha  “NATZI  cha ADOLF HITLER”- Mpaka sasa dalili zote za utawala wa CCM zinafanana na Chama cha Adolf Hitler alipoingia tuu kwenye madaraka 1929 Natzi party  kilianza kuchukuwa power by Force na kuvitumia vyombo vya Dola kama  vile Mahakama, Polisi, Jeshi na Media kumuabudi au kumsifu HITLER. Na Kwa Upande wa UV-CCM kugeuzwa Usalama wa Taifa au Wakuu wa Mikoa, ni dalili ya Utawala mkubwa wa KiDICTATOR unaoendelea kushamiri Tanganyika. Chama cha CCM hakina imani na mtu yoyote yule ambaye atapingana na Utawala wao wa Kimabavu, Ubadhirifu na Kibaguzi.

Kwahivo, Maalim Sefu au Wazanzibari hawakununuliwa na CHADEMA bali Wanayo yadai CHADEMA na Vyama vyengine Vilivoungana na UKAWA ni madai yale yale ambayo Wanayadai Wazanzibari kwa muda wa Miaka 55 sasa. Ndio maana Maalim Sefu ameshikana na viongozi wote wa Tanganyika ambao watakuwa wanatetea Haki , hata kama watakuwa wako CCM- wakiwa na Idea moja yakutaka Muungano wa haki na Utawala wa kuheshimu Katiba za Nchi na Sheria basi hilo ndilo linalowafanya Wazanzibari au maalim Sefu kuwa pamoja na vyama vya Upinzani Tanganyika.

 

CUF KUFA HAITUTISHI WAZANZIBARI

CUF ni Chama ambacho Tanganyika hakipo tena, Kimeuliwa na Lipumba siku ile alipoamuwa kufanya kazi na CCM kwa Ngozi ya CUF na kutumia fedha za Walipa kodi Vibaya. Hivo ningewaomba Watanganyika ambao walikuwa CUF au ikiwa bado wanaiyamini CUF wajiandae kuingia katika Chama cha CHADEMA au  ACT Wazalendo cha Zitto Kabwe- na si Vyenginevo. CUF Tanagnyika haipo tena na wananchi wa CUF kama wanataka haki na maendeleo ya Nchi ambayo yatapatikana kwakutumia Utawala Bora unaoheshimu Sheria na Katiba za Nchi 2 huru. Wafuasi wa CUF TAnganyika wasiangalie kwamba Chadema ni Chama cha Wakristo. Waitizame ChADEMA kama  vile walivokuwa wakiiamini TANU. Ikiwa Watamfuata tena Lipumba 2020, atakuja kuwapeleka kubaya kama vile alivowapeleka mwaka wa 2010 wakati Alipmpigia Debe Jakaya Kikwete wa CCM kwa Waislamu ambao walikuwa CUF. Nakutaka Waislamu wamchaguwe Jakaya Kikwete badala ya Slaa. Huyo Ndie Lipumba ambae alikuwa katibu wa CUF TAIFA 2010.

B. Kwa Upande wa Zanzibar na Wazanzibari, chama cha CUF hata kama kitakufa huku Zanzibar; basi kitakufa katika macho yao tu. Lakini katika Nyoyo za Wazanzibari Chama cha CUF ni Chama cha:-

  1. BISMILLAH
  2. ALLAH KADIRR.
  3. ALLAH KARIIM.
  4. LAA-ILLAHA ILAHA ILALLAH, INNA KUNTU MINAL DHALIIMIN.

 

Wazanzibari ni watu waliodhulumiwa  kwa miaka 55 sasa na   bado wanaendelea kudhulumiwa  na Serikali ya  TANU TANGANYIKA na baadae CCM kwakutumia jina la SMZ. Na katika kipindi hiki choote hatukukata tamaa, kwani tunasimama na nguzo 4 nilizozitaja hapo juu. Na hakika hawatokata tamaa katika Rehma za Allah. Hata Kama Serikali ya TANGANYIKA CCM itakifuta chama cha CUF . Basi katika Nyoyo za Wazanzibari tunachokitaka sio CUF au Vyama ni Zanzibar ilio HURU. Kwa uwezo wa Allah 2020 Zanzibar HURU itapatikana bila yakutumia Vyama vya Siasa au Uchaguzi wa Mizengwe Biidhinillah.

CC wananchi wa Zanzibar tokea mwanzo hatukuwa na imani ya Mahakama za KIMA ambazo zinaendeshwa na MAGORILA.. Ni Maalim Sefu na Viongozi wenzake au wapenzi wa CUF labda ndiop waliokuwa bado wanaimani na Mahakama. Hivo cc wananchi hatuteteruki na tunawaomba CUF wasijale kufutiwa Ruzuku. Hawana haja yakufanya Campeni za Uchaguzi wowote 2020. Nawapumue watuache sasa tudai Nchi yetu ifikapo hio Siku CCM watakapoitisha Uchaguzi.

 

“Innallaha Maa Sabirin”

 

Share: