Habari

WAZANZIBARI: Twa wapongeza Watanganyika/ Tanganyika Taifa Star, kwa Uzalendo mulio onyesha.

Asalamu aleikhum Warahmatullahi ndugu zangu Wazanzibari na Watanganyika wa ndani na nje ya Nchi zetu hizi mbili. Ama mimi namshukuru Allah (SW) kwakunipa uzima na afya yakuweza kuandika makala hii  ya pongezi kwa niaba ya Wazanzibari woote wa ndani na nje ya Visiwa vyetu adhimu. Makala hii nitaigawa katika sub-heading 3:-

  1. Michezo huunganisha Watu na kuleta Uzalendo wa kweli.
  2. Wazanzibari tutabakia kuwa walimu wenu:
  3. Hii ni Tanganyika Star na sio Tanzania Star:

 

  1. Michezo huunganisha watu na kuleta uzalendo wa kweli

Mimi sio mfuatiliaji sana wa michezoi ya mipira ya miguu, lakini inapokuja  ECAC, ACN na World Cup huwa mpenzi mzuri sana ninaefuatilia mpira. Na timu zangu ninazozipenda Offcourse ni Zanzibar katika ligi za ECAC na katika ACN na world cup, timu zangu ni zile za West Africa au nchi nyengine ndogo. Since East Africans team hawajawahi kuingia katika World Cup au African cup of Nation. Let me write what I have aiming for. Nikianzia makala yangu hii yenye kichwa cha habari kama kinavojieleza, sisi Wazanzibari popote pale tulipo tunaungana na jirani zetu na ndugu zetu wa nchi ya  Watanganyika na kufurahia ushindi wa timu yenu hapo jana. Na bila kusahau wananchi wenyewe wa Nchi ya Tanganyika walijitokeza kwa wingi sana katika viwanja na kuwapa ” Full Support”  vijana wenu, HOGERENI SANA

Hakika huu ni uzalendo wa kweli ambao ndani yake nimeona upendo mkubwa miongoni mwa “the Spectators”. Kwa mara ya kwanza wananchi wa Tanganyika, wakubwa na wadogo, kike kiume, kutoka vyama vyote wameacha tofauti zao  na kuwa kitu kimoja ili wafikie malemgo.  Hivi ndivo inavotakiwa, hivi ndivo tunaweza kuzibadilisha nchi zetu na kuwa na democrasia ya kweli na upendo miongoni mwetu. Naamini Umoja huu huu unaweza kuwaletea Watanganyika mabadiliko makubwa ifikapo mwezi wa June wakati timu yenu itakapoingia kwenye mkumbo mwengine wa soka. Na naamini wanaweza kushinda kama wataweka uzalendo mbele. Sisi Wazanzibari tunawapongeza wachezaji wote pamoja na JMP na viongozi wenzake kuonyesha hamasa na upendo katika michezo. Mafanikio hayo ndio chachu yakuwanyanyua Vijana nakuwa na hamu yakujiunga katika michezo mbali mbali ambayo Serikali ya Tanganyika imekuwa ikijivunia fedha zote za Misaada na opportunity zote zinazotokea.

Hata hivo ningewaomba viongozi wa juu wa Serikali ya CCM wasiuchukulie ushindi huu umeletwa na Utawala wa CCM. Ushindi huu umeletwa na vijana wenyewe kwa kuweka uzalendo mbele na kusaidia na Wananchi wote wa Tanganyika. Sisi Wazanzibari inapotokea kheri hatuna Choyo juu ya maendeleo yenu, lakini nyinyi  baadhi  ya Watanganyika hasa katika Idara ya Michezo munakuwa na Chuki kubwa juu ya Ushindi wa Wazanzibari. Naamini ingekuwa ni timu ya Zanzibar ilishinda jana. Basi TFA ingeshapeleka fitina mbele kwa mbele kama ilivo kawaida yenu, hamupendelei maendeleo ya Zanzibar na Wazanzibari. Hapa naandika haya kwa ushahidi wa mifano za fitna zinazotiwa na baadhi ya makocha au  Tanganyika Football Association. Katika mechi ya jana kuna Wazanzibari waliona kwamba mchezaji mmoja Juma Shaabani na Okwi wametupa Magoli kwa Makusudi. Lakini hatuwezi kwenda ACN tukawatilia utambi. Laitani kama ingekuwa haya yametokea kwetu, Mfumo Mzima wa Dola ya Tanganyika na baadhi ya media zao zingetuandama.

 

2. Wazanzibari tutabakia kuwa walimu Wenu:

What can I say… Well!!! Wazanzibari ni walimu wa kila kitu na hii sio siri. Sisi Wazanzibari tunafurahia sana ushindi wenu na uzalendo mulio onyesha. Hongera Umi Mwalimu kwa kelele zako ulizokuwa ukipiga katika Social media, ulikuwa ukiwahimiza watu wajitokeze kwa wingi katika viwanja. Hata kuna siku moja niliona wito wako na nikakujibu kwamba “Uzalendo hauhimizwi ila unakuja natural” . Sasa tumewaona wananchi wa Tanganyika , wakubwa na wadogo, kike kwa kiume wanaanza kuonyesha mapenzi na uzalendo ambao sisi Wazanzibari ndio walimu wenu.

Kwanini nasema sisi Wazanzibari tutabakia kuwa walimu wenu milele?

Wazanzibari wanajuwa kwamba umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, mbele ya neno “TAIFA” ni lazima uamini kwamba hakuna tofauti yoyote katika kujenga taifa hilo.  Either liwe taifa la michezo, taifa la uchumi na maendeleo, taifa la democrasy au taifa la haki sawa kwa kila raia wa taifa hilo. Ni sisi Wazanzibari ndio tuna damu za kizalendo na tumetoa funzo kwenu. Licha ya kwamba mfumo wa mkoloni  Tanganyika zimetufunga kamba za miguu na mikono ili tusifurukute. Lakini tunapigana hivo hivo ili kuwaonyesha  wakandamizaji na wanyanyasaji  wa haki za Wazanzibari kwamba sisi tunaweza kufanya vizuri kama tungefunguliwa pingu za Ukoloni mambo leo. Na tukawa ni mfano ukaigwa na ndugu zetu  wa Tanganyika au jirani wa nchi nyengine za Africa mashariki na kati. Sisi Wazanzibari tunaamini kwamba Uzalendo ulioonyeshwa na Watanganyika pamoja na timu yao na raisi kuwaita Ikulu nakuwapa wachezaji Viwanja ni Wigo kutoka Zanzibar.  Hata hivo, hilo nijambo zuri na la faraja mtu mmoja, kundi au watu kuiga mambo yalio mazuri kuliko mambo mabaya. Hivo basi Wazanzibari wanapoonyesha uzalendo wao juu ya kusimamia kitu wanachokiamini iwe chama cha Siasa, iwe michezo au ushindi fulani wasibugudhiwe na Mfumo katandamizi kwani sisi tunapofanya hivo tunafanya tukiwa na nyoyo safi na hatuna chuki na mtu au taifa lolote lile.

 

 3.Hii ni timu ya Tanganyika Taifa Star na sio Tanzania Star:

Jamani ndugu zangu wa Tanganyika Football Association wacheni ukiritimba wa siasa na mukubali fact kwamba, suali la Michezo halikuwa katika Muungano na maisha halitokuwa katika Muungano huu haramu. Hakuna asiojuwa kwamba Muungano huu ni fichuo kubwa la ulaji wa Rushwa na uporaji wa mali za umma kuzitumia vibaya. Timu yoyote ile iwe imekuwa na sifa zakuitwa “Taifa Star” . Nilazima wachezaje wake wawe wanatoka katika timu mbali mbali za Nchi ya Tanganyika na Zanzibar.  Sio hivo tuu timu hiyo iwe imekusanya wachezaji wa kila Mkoa. Nyinyi Wananchi wa Tanganyika nilazima mulisimamie hili na mulisemee kwa kifua kipana. Kwakuangalia mifano za timu za wenzetu za Taifa jinsi sinavo chagua wachezaji. Mfano Timu ya Uingereza, ina wachezaji kutoka katika mikoa yote ya Nchi ya uigereza tuu. Na timu ya Wales iko hivo hivo hivo na ya Scotland iko hivo. Hawa wana muungano kama huu wa kwetu lakini Nchi zao zinajiwakilisha wenyewe kivyake. Sisi Wazanzibari tumekuwa tukipigwa Chuchuli na TFA kwasababu tuu wanataka kula fedha za michezo na wala nafasi hizo Wazanzibari huwa hawapewi.

Katika timu hii inayoitwa ati Taifa Star, nataka kujuwa muna Wazanzibari wangapi?

Hao Wazanzibari wanatoka katika visiwa vyote vya Unguja na Pemba au laa . Eatlist mukitaka kuturushia changa la macho basi angalau mungechukuwa Wachezaji 2 kutoka kisiwa cha Unguja na 1 kutoka kisiwa cha Pemba. Na hapo Tanganyika mungechukuwa Wachezaji mmoja mmoja kila mkoa. Wengine mungewaweka Banch na wakaingia katika mapumziko.

Critics hii ya Taifa Star inakuja hata kule Zanzibar katika ZFFA, na hawa watu wa Zanzibar Football federation Association nawao ni Wabaguzi kama hawa ZFA. Katika timu ya Zanzibar inayoitwa  ” Zanzibar Herro”  wachezaji wake hawaiwakilishi Visiwa vya Unguja na Pemba. Wachezaji wa Zanzibar Herro ni sawa na hawa Wachezaji wa Kitanganyika wa hii timu wanayoipachika jina la Taifa Star.  Kwa upande wa Zanzibar kuna Ubaguzi wa Upemba na Uunguja ulioletwa na Mkoloni Tanganyika na umeenea hata katika mpira. Wachezaji wa Zanzibar Herro walipokuwa kenya kwenye mechi za East African Cup walionekana kuwa majasiri kwakuwa wachezaji hao hawakuwa wanapumzika na kubadilishana position. Na hii nikutokana na Kuwa hawakuwajumuisha wachezaji wote Wazuri walioko Pemba au sehemu nyengine za Unguja

Hivo Uongozi wa Michezo Tanganyika na Zanzibar ningeomba ubadilishe mfumo wakuchagua Timu za Taifa. Mujuwe kwamba kuna vijana wengi sana katika Mikoa tofauti au vijiji Tofauti wana talent, na wanataka walitumikie Taifa au waendelezwe. Wakati umefika wakuacha chuki katika michezo na kuchagua vijana wazuri wa dogo hata kuanzisha National team ya watoto wadogo ambao baadae watakuja kuchukua nafasi na National Team.

Kwakumalizia ni nasaha zangu kwamba kama timu ya Tannganyika inataka iwe na sifa za Utaifa basi waache siasa katika michezo na waache umimi katika michezo waanze kutembelea mikoa yote ya Unguja na Pemba na Tanganyika kuangalia vijana wazuri ambao wapo. Hawa wanaweza kujenga timu ya taifa star. Na sio kuchukua mchezaji mmoja wa Unguja ambae ana asili ya Bara halafu mukasema timu yenu ni Tanzania Taifa Star. Kama hamuwezi hilo basi timu hii naiitwe Tanganyika Taifa Star na sio Tanzania.

Share: