BarazaniHabari

WAZANZIBARI WENGI WAMEPATIWA VITAMBULISHO

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanya jitihada kubwa ya kuwapatia vitambulisho Wazanzibari miongoni mwa jitihada hizo ni kuhakikisha kila mwenye sifa anasajiliwa na asiyesajiliwa anapatiwa kitambulisho chake, vitambulisho hivyo tangu awali 2005 viligaiwa katika shehia za Unguja na Pemba.

Waziri wa nchi ofisi ya rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, DK Mwinyi Haji Makame wakati akijibu sula aliloulizwa na mwakilishi wa viti Maalum Mwanajuma Mdachi (CUF) huko katika ukumbi wa baRaza la wawakilishi Chukwani Zanzibar.

Mwakilishi huyo aliyetaka kujua kwa nini masheha wana misimamo ya ajabu inaojenga usumbufu wa kupata vitambulisho vya mzanzibari mkazi na kwa nin serikali haifanyi juhudi za makusudi kuhakikisha kuwa wale wote wenye sifa wanapata vitambulisho vyao vya ukaa kabla ya kutengeneza utaratibu wa vitambulisho vyengine.

Mdachi alisema lengo la Serikali kupitia ofisi ya vitambulisho ilifungua afisi katika wilaya zote kumi kwa lengo la kuwafikia kwa karibu wananchi katika kutekeleza hilo serikali imehakikha kwamba Mzanzibari mwenye sifa kwa mujibu wa sheria anapata haki yake hiyo.

Alisema kwa mujibu wa kifungu cha 13(1) (2) kimetoa haki ya kukata rufaa kwa mkuugenzi dhidi ya Afisi usajili na pindipo hajaridhika na uamuzi wa mkurugenzi atakata rufaa kwa mhe Waziri.

Afisi ya Usajili na kadi za Utambulisho Zanzibar inasajili na kutoa vitambulisho kwa Wazanzibari waliotimiza mashati kwa mujibu wa sheria nam 7 ya 2005 pamoja na kanuni iliotungwa chini ya kifungu nam .16 cha sheria hio.

Dk Mwinyihaji, amesema hakuna ukweli wa kuwepo kwa tatizo la kutolewa kwa vitambulisho vya mzanzibari mkaazi kwani kinachojitokeza baadhi ya watu kusajili watoto wasiofikia umri huku wengine wakitumia vyeti feki na kwenda navyo kuchukulia vitambulisho.

Akijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake (CUF) Omar Shehe, Dk Mwinyihaji, zoezi la utoaji wa vitambulisho limekuwa likiendelea hasa kwa upande wa Pemba , ambapo Waziri huyo alisema hoja hiyo haina ukweli kwamba vitambulisho vinatolewa kw aupendeleao kama inavyodaiwa na baadhi ya wawakilishi.

Alisema tatizo liliopo hivi sasa limekuwa likitokana na baadhi ya watu kuamua kuamua kutaka kusajiliwa wakiwa bado hawajatimiza umri unaotakikana kupata kitambulisho hicho huku wengine wakiwa wanatumia vyeti feki.

Alisema hali hiyo ipo kutokana na hivi sasa kuwepo kwa rundo la vyeti feki vilivyokamatwa kutokana na baadhi ya watu kutaka kufanya hadaa ili kupata vitambulisho hivyo kinyume na sheria .

Alisema sio vyema Wajumbe wa Baraza hilo, kujiridhisha na taarifa za watu hao kudai kutopewa vitambulisho hivyo, bila ya kutafuta sababu za msingi ambazo husababisha kutokea kwa mambo hayo.

Akijibu suala la Mwakilishi wa Kuteuliwa na Rais (CCM), Marina Thomas, aliyetaka kujua ni hatua gani serikali inajiandaa kuweza kuwapata watu ambao walisajiliwa na kuacha vitambulisho vyao na namna watavyoweza kuwatafuta,.

Waziri Mwinyihaji alisema tayari kuna mpango ulioandaliwa kutekelezwa kuwasaka wahusika kupitia ngazi za masheha ambapo watafanya kazi hiyo kutokana na baadhi yao ni wenye kufahamika huku wengine wakiwa hawapo nchini kwani wapo wanaoishi Dubai hivi sasa na Uingereza.

Dk Mwinyihaji alisema Usajili huo hufanyika bila mashati ni kwamba mzanzibari mwenye sifa za kisheria hutakiwa kufika mwenye we kwa sheha wa shehia anayoishi kwa lengo la kupata uthibitisho wa uzanzibari mkaazi shehia yake .

Alisema utaatibu huo uko wazi na wala hauna muingiliano na zoezi linaloendelea hivi sasa ni kusajili kwa ajili ya vitambulisho vya mtanzania.

Tagsslider
Share: