Habari

Waziri Aboud awalaumu polisi

IMG_0106
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed amesema wananchi hawana imani tena na Jeshi la Polisi kwa kuwa vitendo vya uhalifu vinafanyika, lakini hakuna wanaotiwa mbaroni badala yake wanakamatwa masheikh na wafuasi wa vyama vya upinzani.
Waziri Aboud alitoa kauli hiyo wakati wa kufunga mkutano wa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi uliokuwa ukifanyika mjini hapa, huku chombo hicho cha dola kikizidi kurushiwa lawama kutokana na ongezeko la uhalifu ambao umefikia hatua ya vituo vya polisi kuvamiwa na askari kuuawa na kuporwa silaha na askari kupiga watu kama pweza.
Jeshi hilo pia linalaumiwa kutokana na jinsi linavyoshindwa kushughulikia vurugu kwa weledi na hivyo kujikuta ikitumia nguvu nyingi zinazosababisha wananchi kuuawa na kujeruhiwa kama vile walivyomuuwa mwandishi Mwandosi na kuwapiga kina Lipumba.
“Tabu inakuja pale uhalifu unapotokea na polisi kushindwa kuwapata wahalifu isipokuwa uhalifu huo unapohusishwa na siasa au dini polisi hawakawii kuwakamata watu wasio na hatia na kuwabambikia kesi, Wananchi wanapenda wahalifu ndio watiwe mbaroni na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia na sio kukamata masheihk wasio na hatia,” alisema Mbunge huyo wa Wara.
Aboud pia aliitaka polisi kujiimarisha katika kusimamia mchakato wa Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa utakaohitimishwa Aprili 30 na Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba kwa kuwadhibiti wale wote wanaoeneza kampeni chafu ya kutaka watu waikatae katiba hiyo kwa kudai kuwa ni uvundo.
“Katika uchaguzi kama huu, kutokea vurugu na kupotea kwa amani, nina imani polisi kuwa wana uwezo mkubwa wa kuzuia hali mbaya isitokee katika uchaguzi kwa kuwashuhulikia wanaopinga katiba pendekezwa,” alisema.
Naye Nkuu wa Jeshi la Polisi, IPG Embe Mango amesema jeshi hilo limejipanga kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani na Kura ya Maoni vinafanyika bila kuwapo na lepe la vurugu ikiwa dalili zitaonesha kuwa CCM inashinda.
“Tunajua kuwa katika matukio ya uchaguzi hutokea uvunjifu wa amani kila wapinzani wanapoona dhahiri kuwa wanaibiwa na pale CCM wanapojiona kuwa wanashindwa, lakini polisi tumejiimarisha katika kusimamia ulinzi na usalama…Tunatamani uchaguzi huu ufanyike kwa amani na utulivu na watu wanyamaze wanapoibiwa kura zao”
Hata hivyo, Mango alisema polisi wamejiwekea mikakati mingi kwa uchaguzi huu wa 2015 baada ya kufanya tathmini na kuona kuna kila uwezekano CCM kushindwa vibaya hasa Zanzibar.
Akizungumzia utendaji, IPG Mango alisema polisi imepunguza makosa mengi ya jinai na ajali za barabarani isipokuwa kilichabaki na namna ya kuwadhibiti wapinzani na masheikh.
Alisema katika mkutano huo wamejitathmini na kujipima na pale palipokuwa na makosa wamejipanga kuyarekebisha ili kwa mwaka huu watimize majukumu yao kwa nidhamu ya hali ya juu. MASHUDU!

Share: