Habari

WEMA yasisitiza watoto kuanzishwa elimu ya Maandalizi

IMEANDIKWA NA MARYAM SALUM, PEMBA

WAZAZI na walezi Kisiwani Pemba, wameshauri kuwaanzisha watoto wao elimu ya maandalizi kwanza, kabla ya kuwapeleka msingi, kwa lengo la kuinua ufahamu wa wao.

Wito huo umetolewa na Afisa Mdhamini wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amani Pemba, kwenye hutuba yake iliosomwa na afiasa wake, Mzee Ali Abdalla, alipokuwa akizungumza na walimu, wazazi walezi wa watoto waskuli ya Maandalizi ya star, atika sherehe za kutimiza miaka kumi ya kuanzishwa kwa skuli hiyo.

Afisa Mdhamini huyo lisema kuwa, umuhimu wa kuwepo kwa skuli za maandalizi kwa watoto, kwanza ni kumfanya mtoto kukua kiakili zaidi, kuwa na uwelewa mpana katika masomo yake mara atakapo anza msingi.

Alisema kuwa, kuwepo kwa skuli hizo kwa sasa katika jamii imeonekana dhahiri kuwa, watoto wengi wanaofaulu skulini ni wale ambao wamepata elimu ya awali kutoka skuli za Maandalizi .

Alisema kuwa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar katika uongozi wa dk. Shein imekuwa ikifuatilia kwa kina sera yake ya mwaka 2006 ya elimu ya kuhakikisha kila mtoto aliefikia umri, anapata elimu kwenye skuli za maandalizi kabla ya kuanza msingi.

Katika hatua nyengine, Mwakilishi huyo wa Afisa Mdhamini, m aliwataka walimu na mwalimu wa mkuu wa skuli hiyo ya Star, kujiwekea mipango yao vizuri, hasa katika suala la ada zao za skuli na kufuata mitaala ya wizara ya elimu ili kwenda sambamba hapa nchini.

Nae Shuwena Mahamoud Ali mwalimu wa skuli hiyo akisoma risala, alieleza kuwa skuli yao inakabiliwa na uhaba wa madarasa hasa ya msingi, hivyo ni vyema kwa wizzara ya Elimu, kuwapatia eneo ama jengo japo chakavu, ili walifanyie uakrabati na kukidhi haja.

Hata hivyo mwalimu huyo alieleza, awali skuli hiyo ilianza kwa dhana ya kibiashara, ingawa kwa sasa haipo kibiashara zaidi ipo kutoa elimu bora.

Kwa upande wake mwalimu mkuu skuli hiyo Moza Said Salim, alitoa wito kwa wazazi walezi kutoa ushirikiano kwa walimu, kwani wamekuwa wakikabiliwa na changamoto katika kazi zao.

Alisema lengo la skuli yake ni kuona inatoa wanafunzi walio bora kielimu, hivyo ili kufikia hilo lazima wazazi na walezi, wawe karibu na skuli hiyo.

Skuli ya Maandalizi ya Star, ilipo kichungwani Chakechake kisiwani Pemba, imeanzishwa mwaka 2009, ikiwa na walimu wawili ,ambapo hadi kufikia sasa skuli hiyo imekua na walimu saba, wananfunzi 179, pamoja na madarasa sita yakiwemo matatu ya nasari na matatu ya junior .

MWISHO.

PembaToday

Share: