Habari

Wengine watatu wanaodaiwa kutekwa Mtambwe wapatikana, wakamilisha idadi ya watu sita

April 15, 2018

Imeandikwa na Mwandishi wetu Pemba.

Watu watatu wengine kati ya wale sita waliyodaiwa kutekwa na kuchukuliwa na watu wasiojuulikana wameokotwa saa 8 usiku wa kuamkia leo katika maeneo tofauti huku hali zao zikielezwa kuwa ni mbaya na hivi sasa wapo hospitali ya wete wakiendelea kupata matitabu.

Watatu hawa na wale waliosalia kati wa watatu walioachiwa hivi majuzi

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kiongozi wa wa jumuiya ya vijana CUF Mtambwe ndg ; Mohd Khatib amesema vijana hao wameokotwa katika maeneo tofauti ambapo wawili kati yao waliokotwa Mzambarauni na mmoja ameokotwa Likoni njia ya kuvukia kuelekea kojani.

” Mzambarauni waliokotwa Thuwein Nassor Hemed pamoja na Khamis Abdalla Mattar na Likoni aliokotwa Khalid Khamis Hassan” alisema Mohd

Nd Mohd amesema , kutokana na doria maalum waliyokua wakiifanya wananchi wa jimbo la Mtambwe ndio kulikofanikisha kuonekana kwa vijana hao ambapo amesema vijana wa doria walishitushwa kuiona gari isiyokua na nambari ikitembea hivyo kuitilia mashaka na walipoanza kuifatilia waliikosa kidogo lakini na baadae ndipo walipowaona watu hao wakiwa washatupwa.

Akizungumzia hali za watu hao amesema , bado afya zao si za kuridhisha kwa sababu hawawezi hata kuzungumza na miguu imewavimba kiasa ambacho hawawezi hata kusimama.

Nae Saidi Nassor Hemed ambae ni kaka wa Tuhuweini Nassor Hemed amesema hali sio nzuri kwani hadi muda huu wapo katika hospitali na watu wao hawawezi kuzngumza ” hali zao ni mbaya , hawawezi kuzungumza , wamekonda sana lakini katika migongo yao wanamakovu mengi ya kupigwa na kitu kama waya hivi ” alisema Said.

Aidha amesema kuwa watu hao wanaharisha damu na wanakwenda haja ndogo yenye kutoka sambamba na damu.

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini Pemba Haji Khamis Haji amethitibisha kupatika kwa vijana hao ambapo amesema bado hawajapata maelezo ya vijana hao kutokana na kuwa katika harakati za kimatibabu.

” tutakapo tuzungumza nao ndio tutajua nini kinaendelea lakni mpaka sasa wapo hospitali wanaendelea na matibabu ” alisema kamanda huyo

Pembatoday

Share:

1 comment

 1. chatumpevu chatumpevu 15 Aprili, 2018 at 11:27 Jibu

  Wazalaendo

  Bila ya kupepesa macho waliowateka wenzetu sita ni vikosi vya smz wakishirikiana na TISS ( usalama wa taifa). tukio hili la kikatili ni wake up call ( uamsho) ili tujue kuwa kuna wabaya wengi wasioitakia mema Unguja na pemba. Watekaji hawa ni sehemu ya kundi kubwa la maharamia na wauwaji waliotoka bara ili kuja kuungana na watesaji na watekaji walioko znz kutoka vikosi vya smz vinavyopata amri kutoka kwa nduli Haji Omar Kheir kwa minajili ya kuwatia adabu wazanzibari . Ushauri wangu ni kuwa wazanzibari tukio hili liwe la mwisho kwa maana kuwa katika maeneo yetu tunayokaa tuweke vikundi vya ulinzi na tuwe na tufanye njia yoyote tumiliki bunduki kubwa na vipaja vya kuku wa malawi vyenye kubeba njugu zaidi ya 15 for self defence kwa sababu hawa wanapokuja huja na vitu vya mtoto ( SMG) na silaha nyengine za kijadi, mapanga, pinde, nk. Silaha hizo hakuna haja ya kuzisajili ( hapa nafuta kauli yngu ya zamani kuwa zisajiliwe) wanapokuja ktk maeneo ya makaazi waamini kuwa wananchi hawajajitayarisha. chengine ni kuwa wanapikuja na magari yao basi kuwe na wengine wafanye inavyowezekana magari wayatie moto ili wasiweze kurudi walikotoka, na huku wananchi wengine wakijiandaa kuwa na mapanga na kila aina ya silaha. Kwa sababu katika mfumo wa serikali iliyo makini haiendeshi mambo yake ya kiulinzi kwa utaratibu huu wa utekaji na kuumiza raia wake. Huu ni utaratibu unaotumia na wahuni na majambazi. Serikali hufanya mambo yake very formal . na kama wabaya hawa wanakuja kwa njia hiyo ya utekekaji basi ni lazima wananchi nao wajitayarishe kukabiliana na majambazi hao kwani mara zote inapotokea hivyo serikali hukanusha kuwa wao hawahusiki na kama hawahusiki basi ni majambazi ndio wanaofanya vitendo hivyo kwa hivyo ni haki kwa wananchi kuwashughulikia majambazi hao wanaotumwa na serikali squarely. sasa inaelekea kuwa dola inaletea ubabe dhidi ya raia wake na hapana budi wananchi nao wajilinde kwa njia zozte wanazoweza kuzitumia.

  Inapendekeza kama kuna movements ambazo si za kawaida basi wananchi waweze kupeana taarifa haraka inavyowezekana na ikibidi watumie hata neno la password kam vile ambayo kwenye vita wanajeshi wanavyotumia passwords wakiwa makambini kusudui tu mashushushu waliopoandikizwa miongoni mwa wananchi wasiweze kuelewa kitu gani kinapangwa.

  Imefika wakati sasa wananchi Unguja na pemba wajilinde wenyewe kwni dola badala ya kuwalinda wananchi na mali zao imekuwa ndio inayoanya ugaidi dhidi ya raia wake wasio na hatia. Naomba nitoe kisa kimoja miaka ya 2002 nilikaa moja ya mitaa ya Unguja na kwa bahati kulikuwa na kikundi cha wahalifu waliokuwa wakivunja milango kwa kutuma jiwe kubwa lililokuwa likiitwa Fatma. Wengi waliathirika na visa vile hususan wanawake kwa sababu wako waliobakwa na wahuni wale walikuwa wakishavunja mlango na wakiingia ndani walikuwa wakimweka mwanamme chini ya ulinzi na kuwaharibu wanawake. Sasa mitaa mitatu ikakutana na kujadili namna ya kuondoa kabisa uhuni ule. Moja lililokubaliwa ilikuwa ni kuweka doaria na kupeana neno la password. Ikatokea siku moja wahuni wakaingia kwenye mita 18 , na kama saa nane ucku tuliokuwa katika doira tukaona wahuni 6 wanakuja wakiwa na mapanga, mmoja kati ya waliokuwa ktk doria akawasimamisha na kuwauliza nyinyi ni nani na mnaenda wapi? kuuliza vile wahuni wakamtolea panga na jamaa akatamka neno la password na ghafla umati mkubwa kutoka migombani na vichochoroni uliwazunguka na kuwashambulia wahuni wale hadi kuzimu wote sita. Tokea siku hiyo visa na mikasa vilikoma na tuliendelea kulala kwa amani hata ukiacha mlango wako wazi maana wezi na wahuni walikuwa wakiambizana kuwa mitaa ile bwana usipite kabisa usiku mkubwa.

  Sasa ndugu zangu huu ni wakati wa kuchukua jukumu la ulinzi mikoni mwa wananchi baada ya serikali kushindwa kuwalinda raia zake.

Leave a reply