Habari

Wizara ya Afaya yatoa Tahadhari na kimeta

Na Fatma Kassim, Maelezo

Wizara ya Afya imetoa tahadhari kwa wananchi na wafugaji wanyama kuwa wangalifu na maambukizi ya ugonjwa wa kimeta unaoambukizwa na wanayama baada ya taarifa za kuibuka ugonjwa huo kaskazini mwa tanzania bara.

Mkuu wa kitengo cha kuzuia na kudhibiti  maradhi yakuambukiza na yasiyoambukiza dr salma masauni amesema  taarifa za shirika la  afya duniani who tanzania  imeeleza kuwa ugonjwa huo umeibuka  mwezi uliopita katika kijiji cha kitunda  mkoani kilimanjaro na hadi machi 10 wagonjwa kumi wamebainika na mtu mmoja amefariki dunia.

Ugonjwa huo wa kimeta unaoambukiza binaadamu kwa njia ya hewa ,kula au kutafunwa na mnyama aliethirika  miongoni mwa dalili zake ni kutapika na kuharisha ,kukausha damu uvimbe wa ngozi na kupoteza hamu ya kula .

Hata hivyo dk salma alisema  kwa sasa ugonjwa huo haupo zanzibar ila ni vyema kuchukuliwa tahadjari kwani ni miongoni mwa magonjwa yasiyonamipaka yanayoambukiza kutoka kwa wanyama.

Alisema  wafugaji wa wanyama wakiwemo ng’ombe mbuzi ,kondoo  wanapaswa kuchukuwa tahadhari  hasa kwa kuwapatia wanyama wao chanjo  kwani wanaweza kuathirika na kuambikiza ugonjwa huo wa kimeta.

Aidha amewataka wananchi kuchukuwa tahadhari yakununua nyama sehemu zinazotambulika  pamoja na kutoa taarifa katika idara ya mifugo na wizara ya afya ili kuchukuliwa hatua za haraka iwapo watakuta mzoga wa mnyama umefariki.

Amesema   wizara  hiyo kwa kushikiana na idara ya mifugo  wanatarajia kukaa  pamoja kujadili njia za  kukabiliana na ugonjwa huo iwapo utagundilika nchini na hatua ya awali ni kutoa taaluma kwa jamii juu ya kimeta.

Nae  Dk mkuu wa mifugo wa  idara utabibu na mifugo talib saleh suleiman imesema kuwa katika hatua za awali za kuzuia wamepiga marufuku uingiaji wa wanyama wa aina hiyo kutoka katika mkoa wa kilimanjaro ambao kumekuwepo  kwa ugonjwa huo.

Amewashauri wanaoingiza wanyama kutoka tanzania bara wasichukue mifugo katika maeneo yaliyoathirika na kimeta na kuwasisitiza  kufuata maelekezo ya uchukuaji ya wanyama hao kuleta hapa nchini.

Kwa zanzibar ugonjwa huo ulijitokeza zaidi ya miaka kumi nyuma na ngombe mmoja alibainika kuwa na ugonjwa huo katika maeneo ya fuoni.

 

Share: