Habari

zanzibar chini ya muungano wa mkatabaa

http://blip.tv/mzalendonet/kama-tulivyouwa-a-s-p-na-tanu-tukazaa-ccm-na-tuuwe-huu-tuuzae-mpya-muungano-6463398

Zanzibar yenye Malaka Kamili Kitaifa na Kimataifa ikifuatiwa na Muungano wa Mkataba na Tanganyika itaitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na italinda na kuheshimu yafuatayo:

Zanzibar itakuwa ni Nchi ya Kidemokrasia.

Zanzibar italinda na kuheshimu haki za binaadam.

Zanzibar italinda haki za makundi mbalimbali na makundi yenye mahitaji maalum.

Zanzibar itaridhia Mikataba mbalimbali ya kimataifa.

Zanzibar itapinga ugaidi.

Zanzibar haitokuwa chaka la magaidi.

Zanzibar itapiga vita madawa ya kulevya.

Zanzibar itajiunga na Jumuiya za Kikanda na Jumuiya za Kimataifa.

Zanzibar haitoruhusu ardhi yake itumike kushambulia Nchi jirani.

Zanzibar itaendelea kuwa mlizi wa Mwambao wa Afrika Mashariki.

Zanzibar haitokuwa chaka la magaidi.

Zanzibar italinda haki ya kuabudu.

Zanzibar itaruhusu vyama vya siasa na Mgombeya Binafsi.

Zanzibar haitoingilia Uhuru wa Mahkama.

Zanzibar Mamlaka ya kuendesha nchi yatakuwa mikononi mwa wananchi.

Zanzibar itaheshimu vyombo vya habari.

Zanzibar itaheshimu Uhuru wa kujieleza, uhuru wa mawazo na maoni.

Zanzibar itarudisha hadhi yake ya kuwa kitovu cha elimu.

Zanzibar itakuwa ni kituo cha biashara duniyani.

Zanzibar ni njema mwenye heshima zake aje.

Zanzibar itayahashimu haya na mengine kama haya ilikuendena na mahitaji ya duniya ya sasa.

Jamhuri ya Watu wa Zanzibar – KWANZA!

Share: