Habari

Zanzibar Elections: uchaguzi umeanza vyema, licha ya…

Alhamdullillah, tumeamka salama leo ikiwa siku ya Jumapili tarehe 25 October 2015, siku ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar na Tanzania. Leo ni siku ambayo Wazanzibar na Watanzania wameamka na moyo wa matumaini ya kufany mabadiliko ya mfumo wao wa kujiongoza.

Kazi hii imepiganiwa miaka mingi iliyopita, ambapo, kila inapotokezea fursa hii Wazanzibar wamekuwa wakifutwa matumaini yao. Utashangaa vipi matumaini hayo yamekuwa yakirudi zaidi mwanzo ulivyokuwa.

Kwa jumla kazi ya upigaji kura imeanza vyema, kama kawaida ya binaadamu kasoro zinakuwepo.

Hadi sasa hakuja ripotiwa serious problem. Vituo takriban vyote vimefunguliwa kwa wakati, wananchi wamejitokeza kwa wingi na kwa utulivu, kila mmoja akimaliza kupiga kura yake anaondoka.

Zipo taarifa zisizo rasmi kuwa baadhi ya vituo vifaa vya kura vya NEC vimechelewa kidogo, lakini haiwezi kuathiri kiasi kikubwa upigaji kura.

Tukiwa na mtandao wa Observer 20, tutakuwa tunawajuvya hatua kwa hatua za uchaguzi zinavyoendelea.

Na wewe mzalendo usiache kutuandikia au kutujuvya chochote kile chenye faida katika uchaguzi huu.

Salam kwako Maalim Kisisina

Share: