Habari

zanzibar huru yenye mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa, coming soon

visiwa vya zanzibar ni vidogo sana na ni vvenye utajiri na rasilimali kubwa sana, raiya wake ni wachache mno, cha kushangaza ni kua hakuna maendeleo kila kukicha afadhali ya jana, sekta ya afya katika hospitali hakuna dawa hakuna huduma bora inayo stahili kwa binadamu, elimu imezoifishwa, viwanda ajira hakuna vijana wote washaota mvi washazeeka wengine wamejiingiza kwenye utumiaji madawa ya kulevya kutokana na mawimbi na msongamano makubwa ya mawazo ya kimaisha mtu unaamka asubuhi hujui ulekee wapi, vijana ambao ni nguvu kazi ya kesho wanaasirika kisaikolojia, walobahatika kuoa na kuzaa watoto basi pia hawana matunzo mazuri na watoto wao kutokana na njaa na matatizo ya kuwapa elimu bora watoto wao, hawajui nini wafanye mana hata kijio kinawashinda utamkuta mtu njiani unapishana nae anaongea peke yake utazani chizi kumbe ni mzima milo mitatu inawashinda wananchi wengi sana zanzibar kutokana na ugumu wa maisha walonao, wanaoishi kwa raha na furaha ni viongozi wa serikali tu, wao na familia zao watoto wao huwapeleka njee na nchi kupata elimu bora huduma bora za afya, tujiulize wazazibar tumeishi na serikali ya mapinduzi CCM kwa kipindi cha miaka 50 bado hali ni hio hio na inazidi kua hivo, sasa tutafakari kisha tujipe majibu, kama kuwachagua viongozi wa ccm tumeshawachagua sana hakuna lilokua,ispokua nchi kuweka pabaya wakiwa wao ndio tulowakabidhi uongozi na kuilinda na kuitetea nchi yetu, na inaonesha wazi kua hawana nia njema kiukweli viongozi wa ccm hapa zanzibar wanawafanya wanachi wao kama ndondocha, sasa basi tusiwe tena wapumbavu, ikifika octobar tufanye mamuzi ya kuikataa ccm, kwa hali yeyote liwalo na liwe tutizamewajibu wetu kiungalifu tusidanganyike tena tuinusuru zanzibar yetu kuokoa vizazi vyetu vya badae,tuamue na kuangalia hali ya upande mwengine inshallah kheir,

Share: