Habari

Zanzibar na harakati za utafutaji mafuta na gas asilia sehemu 2

Inatoka sehemu ya Kwanza…..

Suala la utafutaji was mafuta na gas asilia likiendelea nchini kwetu Zanzibar, tunaangalia makundi matatu muhimu kufanikisha utafiti huu, ambayo ni serikali, makampuni ya mafuta, na taasisi za kiraia.

Fungu la NNE ambalo ni wananchi wenyewe, kwenye mtiririko huu nitaliacha mwiku.

Leo nitaanza na kampuni za utafutaji mafuta kama ilivyo kawaida yetu hakuna taarifa za kutosha. Ninavyotambua eneo la kitalu cha Zanzibar lipo mikononi mwa kampuni ya Antrim ya Canada tokea mwaka 1997. Baadae wakaingia ubia na Kampuni ya RAK kutoka nchini ya Ras alkheima.

Kwenye suala la mafuta kunahitaji uwazi wa hali ya juu kila hatua inayofanyika. Ipo haja ya kufahamishwa wananchi kila kampuni inapokabidhiwa jukumu lake.

Nchini Nigeria kutokana na kutokuwa na uwazi suala la mafuta lilisababisha uhasama mkubwa baina ya wananchi wa kabila la Ogadeni na serikali Yao. Uhasama huu ulipelekea kuuwawa na kunyongwa kwa watu mashuhuri Kama Ken Sarawiwa.

Nimefuatilia suala la wafanya kazi wa kampuni hizi hakuna Wazanzibar. Ninavyo fahamu kipindi cha miaka 10 iliyopita serikali ilianza kujikita kusomesha vijana wa Kizanzibar somo la Mafuta na gas. Nataka tuone tunaiutumia fursa hii kuwaingiza vijana wetu kazini. Hili liwe fanikio jengine kupitia mafuta na gas.

Taarifa za kampuni za utafutaji mafuta ziwekwe wazi, nafasi za kazi zitangazwe, wananchi wanufaike tokea hatua ya mwanzo ya maendeleo ya mafuta. Kampuni za utafutaji mafuta tokea awali zitenge mfuko wa maendeleo ya jamii. Mfuko huo uanze kazi sambamba na utafutaji wa mafuta ukiendelea. Isisubiriwe Hadi dakika ya mwisho kungoja ushahidi kamili.

Taasisi za Kiraia
Nimeulizia uwepo wa taasisi za Kiraia zinazo zungumzia masuala mafuta. Bado wasomi wetu wapo nyuma. Taasisi za Kiraia ambazo zimeanzishwa ni kampuni zinazofanya kazi kwa maslahi binafsi. Taasisi nyengine ni zile za mazingira ambazo hujipenyeza kwa mwemvuli huo.

Tulizowea kupaza sauti zetu za maendeleo ya mafuta kupitia chama cha kisiasa- CUF. Leo hii CUF imezongwa na mambo yake, haipati tena kilisemea suala la mafuta.

Lakini kwa upande mwengine ipo haja kiiweka CUF kwenye suala hili. Badala yake tuwe na sauti ya umoja bila kujali mirengo kwa maslahi ya jamii na nchi yetu.

Hivyo basi tunahitaji kuwa na taasisi imara zenye utaalamu na weledi kwa sector nzima ya mafuta. Tukumbuke kuwa suala la mafuta ni complex issue, inachukuwa muda mrefu, utaalamu, gharama, ujumuishaji wa sector chungu nzima, etc.

Ukizungumza na wananchi sasa hivi utaona tayari kuna gap, wamekosa maelezo. wapo wanaoishi kwa khofu, wapo wanaodhani kesho watahamishwa majumbani mwao. Haya yote nimeelezwa personal na wananchi wenyewe. Taarifa kubwa waliyopewa no kuangushwa vikaratasi, basi. Bahati sikupata copy yake.

Tujenge msingi bora wa maendeleo ya mafuta Tokea leo

Share: