Habari

Zanzibar na harakati za utafutaji mafuta na gas asilia

Nimeshuhudia kwa macho yangu kila unapopita barabarani kuona harakati za magari ya kiraia kubeba bendera nyekundu.

Mwanzo nilishtuka, kwani nilishazowea kuona gari za kijeshi ndio zinazo beba bendera nyekundu tena wakati wa dharura. Leo ni kinyume chake, sasa ni gari za binafsi. Ilivyo nipitikia akilini mwangu nikuwa vikosi vya kijeshi sasa vinatumia gari binafsi.

Nilivyo fanya upekenyuzi nikaambiwa hapana, zile sio gari za vikosi bali zile ni gari za kampuni za utafutaji wa mafuta na gas asilia hapa Zanzibar. Na kwanini zinabeba bendera nyekundu, jawabu nikuwa mafuta ni mambo ya hatari ndio gari zote zikabeba bendera nyekundu.

Kwa ufupi hiyo ndio dhana iliyopo ndani ya vichwa vya watu wakati zowezi la Utafutaji mafuta likiendelea.

Nataka niangaze mafungu matatu katika katika mchakato huu, ambayo ni serikali, kampuni za utafutaji mafuta na taasisi za kijamii juu ya utafutaji mafuta.

Serikali yetu bado ipo chini ya minyororo kuhusiana na suala zima la utafutaji mafuta nchini Zanzibar. Kutokana na kubanwa na sheria za mafuta za Tanganyika bado haijaweza kufurukuta licha ya juhudi dhaifu zilizofanyika. Kwangu mimi ni mtego wa kikoloni tu kutaka Zanzibar ifanye utafutaji wa mafuta ikitumainiwa kuwa asilimia kubwa Zanzibar ndio kwenye mafuta. Baadae kutumia ukoloni huohuo kuyadhibiti mafuta pale yatakapo patikana kama vile zilivyo dhibitiwa sector nyengine zilizo chini ya mamlaka yake.

Mfano TCRA sasa hivi inaidhibiti hata ZBC, mambo ya IT, Spectrum, wakati yote hayo hayamo kwenye orodha. Imejibadili kutoka Regulatory sasa imekuwa Authority. NECTA imeishikillia elimu ya secondary wakati haimo kwenye mamlaka yake. Halkadhalika Zanzibar inayo baraza lake la mitihani.

Kwenye suala la mafuta kwa vile sheria hazija badilika mwisho wake itakuwa hivyo hivyo.

Jengine nikuwa hilo shirika la maendeleo ya mafuta Zanzibar sijuwi niseme hawana uwezo, changa, ndio kwanza, ilhal neno lolote utakalo tumia linakhalis mwenendo wake. Husikii kujikurupusha kwa kutunga sheria, uajiri, na kutowa elimu kwa raia. Nimefuatilia kuna baadhi ya vijana walioahidiwa kuajiriwa lakini unaona kabisa uimarishaji wa shirika hauendi sambamba na speed ya utafutaji. Utafutaji uko mbele shirika liko nyuma, mwisho wa siku ni kampuni za mafuta ndio zitakazo nufaika.

Licha ya kupewa Mkurugenzi mpya bado hajawa na uzowefu, kujiamini na speed ya kuendesha shirika. Bado Mkurugenzi huyu anatumikia kama aliyeajiriwa na TPDC (Tanzania Petroleum Development Corporation)

Inaendelea…….

Share: