Habari

Zanzibar sio nchi,dola wala nchi huru

Imekuwa ikisemekana zanzibar ni nchi lakini hivi karibuni imegundulika sio nchi, wala dola, wala nchi iliyo huru bali ni sehemu ya Jamhuri ya muungano wa tanzania au unaweza kusema ni eneo la Tanzania au mkoa wa Tanzania au jimbo la tanzania

Hiyo bendera waliyonayo, wimbo walionao na rais wanaemchagua ni geresha tu

Wiki iliyopita wakati CAF wakiifutia zanzibar uanachama walihoji kama kuna nchi duniani inaitwa zanzibar inayojitegemea na mambo yake binafsi kama sudani kusini

Wakaangalia na ramani ya dunia kama kuna nchi inaitwa zanzibar hawakuiona bali waliishia kuiona Tanzania tu

So wale wanaosema zanzibar ni nchi hili wanalitoa wapi? Kama dunia haijui kuna nchi inaitwa zanzibar bali ni sehemu ya tanzania

Huu urais huko zanzibar Na bendera waliyo nayo na wimbo walionao unawasaidiaje kuwa nchi inayotambulika?

Yangu macho.

kutoka kwa Eden Kimario wa jamii forum

Share: