HabariMichezo

ZANZIBAR YAFUNGULIWA MLANGO #CAF

#ZANZIBAR YAFUNGULIWA MLANGO #CAF

Alhamdulillah leo #Zanzibar tumepiga hatua moja mbele. Nami napenda niungane na wenzangu kulifurahia hili na kuwapongeza wale wote waliosimamia na kupiga kampeni, rasmi Zanzibar ni mwanachama wa 55 #CAF (Shirikisho la mpira wa miguu Afrika). Pamoja na furaha yetu naomba kidogo tulizime hili dufu tujiulize maswali yafuatayo:-
1)Tanzania itawakishwa na nchi mbili, suala la kujiuliza hapa ni nchi zipi #Zanzibar na #Tanganyika? au Zanzibar na Tanzania?

Maana hata kwenye mtandao wa #CAF wameweka picha inayoonesha bendera na jina la Tanzania ambayo kisheria unaposema Tanzania maana yake Zanzibar imo humo ndani. Kisha kwa chini yake “kama picha inavyojionesha” imewekwa Zanzibar kwa jina lake na hiyo bendera yake (iliobuniwa hivi miaka ya karibuni)

2) Kwenye mashindano ya #CECAFA ambayo hayatambulikani na #FIFA Zanzibar inashiriki sambamba na Tanganyika pia lakini swali linakuja hapa, Tanganyika inaingia kwa jina la Tanzania Bara na bendera inatumia ya Tanzania sasa tuseme Tanzania Bara (kama wanavyojiita) hawana bendera?

3) Vipi kuhusu suala la ligi. Au Tutaendelea kuwa na ligi ya Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara?

4) hali itakuwaje kwenye mashindano ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu. Zanzibar itapewa fursa ya kushiriki mashindano ya klabu bingwa barani Afrika au itaendelea kupewa ubamba wa kunde kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho?

5) na wimbo wa taifa nao ni alama muhimu mchezoni hasa katika mashindano ya ngazi Taifa, #Zanzibar tunao wimbo wa taifa je Tanganyika wanao na kama wanao wanautumia?

FB

Share: