Habari

ZANZIBAR YAWEKWA UTUMWANI KWA MIAKA 54

DONDOO MUHIMU KUELEKEA TAREHE 26 APRIL SIKU AMBAYO WAZANZIBARI TULIPOTEZA UTAIFA WETU

ZANZIBAR YAWEKWA UTUMWANI KWA MIAKA 54

Katika kitabu kinachoitwa “Wasifu wa mlinzi wa kwanza wa Mwalimu Nyerere (1960-1973) kilichoandikwa na Bw. Peter D. M Bwimbo na kuchapishwa na Mkuki na Nyota Publishers LTD.

Muandishi katika ukarasa wa 47 anasema Mwalimu Nyerere aliwahi kusema:

“Kutawaliwa na Taifa jengine kwa nguvu sio tu kwamba ni fedheha bali pia ni sawa na kuwekwa katika utumwa”

Aliendelea kusema kuwa ni wajibu wa watumwa na vijakazi tu kushangiria makosa ya wakubwa zao, lakini mtu huru hawezi kushangiria makosa ya wakubwa zake.

Kwa Wazanzibari kusherehekea siku ya kuuwawa kwa Dola ya Zanzibar (26/April/1964) sio tu ni kushangiria makosa yaliyofanywa na wakubwa wetu waliopita bali pia ni kuendeleza khulka na fikra za kitumwa.

Kinachonisikitisha na kunitia simanzi ni kwamba pamoja na mapinduzi mwaka 1964 ili tujitawale wenyewe Wazanzibari kumbe hadi leo tumo na tunao watu wanaoendeleza fikra na khulka za kitumwa.

#AjendaYaZanzibar

– kwa hisani ya Hafidh Ally.

Share: