Habari

ZATU si chama cha kisiasa

March 11, 2018

Chama cha walimu Zanzibar zatu kimesema kitaendelea kupigania maslahi ya walimu nchni pamoja na kulinda hadhi ya walimu ambayo imeonekana kushuka kutokana na matatizo mbalimbali.

Akizungumza na Zanzibar24 Wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo wa utendaji viongozi wapya waliochaguliwa kwa ajili ya kuwaongoza wanachama katika chama hicho Katibu Mkuu wa chama cha walimu Mussa Omar Tafurwa amesema lengo kuu la kuanzishwa chama hicho ni kutetea maslahi ya walimu nchni lakini wapo baadhi yao hukishirikisha chama hicho katika misingi ya kisiasa jambo ambalo ni kosa kisheria kwani chama hicho hakipo kisiasa kama baadhi yao wanavyodhani.

Amesema ili kwenda sawa na sheria pamoja na kanuni zilizopo chama hakita kumvulia mwanachama yoyote atakae bainika kuvunja maadili ya chama hicho kwa kujiingiza katika siasa, ambapo amesema kwa hatua za awali atakapo bainika kiongozi atasimamishwa uongozi au kuachishwa kazi moja kwa moja.

Kwaupande wao baadhi ya Viongozi Waliopatiwa mafunzo hayo ya uongozi wameahidi kufanya kazi kwa mujibu wa sheria pamoja na kufuata miko na maadili ya chama ili lengo la chama hicho liweze kutimia na kutoa wito kwa wezao kuzidisha bidii katika kutoa taalum na kuwachana na itikadi za kisiasa ambazo zinaweza kukatisha njiani ndoto cha chama hizo.

Chama cha walimu zatu kimeandaa mafunzo hayo ya siku tatu kwa walimu ambao ni viongozi wapya waliochaguliwa ili kutetea maslahi ya walimu wa Zanzibar.

Pembatoday

Share: