ZenjiLikiz

Joto la uchaguzi lazidi kuwatesa ccm, kuna tetesi huenda Uchaguzi mkuu 2015 ukafanyika Z’bar tu wa Raisi Znz na Wawakilishi

Kuna tarifa za tetesi kutoka kwa makada wa ccm na mikakati yao ya mbinu gani ili waweze kupita salama katika uchaguzi mkuu wa mwaka oct2015 ? katika panga pangua yao , na tetesi zilizopo nikua uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2015 ni mzito kwa pande zotembili za Muungano katika chaguzi zote tokea kuingia mfumo wa vyama vingi Tanzania.

Kwahali hio ccm hivi sasa wanapanga wakipangua ni njia gani watumie ili waendelee kutawala? Tetesi zilizopo ambazo tayari makada wa ccm wanazieleza nikua huenda uchaguzi mkuu wa 2015 ukafanywa kwa upande moja tu wa Zanzibar Uraisi wa Smz na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi .

Hii eti nikupunguza joto kwanza la upande moja na kujipanga kwa uchaguzi mwengine wa Muungano ambao huenda ukafanyika 2018, kwa mujibu wa wenyewe ccm na mipango yao ,nikua eti uchaguzi wa Zanzibar huto asiri uchaguzi wa Muungano pindipo ukifanyika wa Zanzibar.

Share: