ZenjiLikiz

Madda Iliyoingia Shadda

Nafikiri wenzangu mutakuwa mushaiona document hii:

IMG-20130225-WA0004

Suali, sisi tusio wakristo wala tusio na asili ya Tanganyika, tumeupataje waraka huu? Jawabu ni rahisi tu. Kwamba sio kila mkiristo au kila mwenye asili ya Tanganyika hana utu wala ustaarabu. La hasha nakataa. Wao kama ni binaadamu wameumbwa sawa na binaadamu wengine na hivyo wako wengi wenye kututakia kheri na wako wengi wasiotaka ‘mambo ya kigaidi’ kufanyika hapa visiwani petu la kwao Tanganyika. Kwa ufupi ni watu wanaopendelea kupigania haki, usalama, amani, na utulivu wa nchi.

Hypothesis A – Haiwi kuwa kupenya kwa waraka huu ukawa ni sababu ya mauwaji yanayotokea hivi sasa Zanzibar?

Wazanzibari tunajijua vyema. Hatuna sifa za ‘unyama’ wa kuuana kama kuku. Si leo, si jana, si juzi. Maadili yetu yameoteana ndani ya tabia zetu kwamba kumwua hata mnyama tunaona jambo zito. Wengapi kati yetu tunaona shida kumwona mnyama kuchinwa? Sikwambii binadamu.

Lakini historia inatwambia kwamba mauaji mengi yaliyofanyika visiwani humu yamefanywa na watu wasio na asili ya Zanzibar. Vishindo vya Juni 1960 vilikuwa ni watu kuto nje ya Zanzibar. Yanayoitwa mapinduzi hali kadhalika ni watu kutoka Uganda , Kenya, na Tanganyika (hususan Tanga) ndio wenyewe na WACHINJAJI wanajulikana. Hata marehemu mzee Karume mwenyewe ameungama na jambo hili pale aliposema yeye hakupindua kapewa tu serikali aendeshe. Hata vita maarufu hapa visiwani vijuilikananvyo kama vita vya Wamanga na Washihiri waliopigana hawakuwaWaswahili wa Kizanzibari pia. Ni watu kutoka Umangani na Ushihirini ambao akthari yao hata Kiswahili chao cha matata.

Kwa hili la sasa inaonesha dhahiri kutokana na waraka huu kwamba ni tena watu ambao hawana uchungu wala imani ya Zanzibar wanataka kutuletea mauaji yasiyoelekea. Ni kweli kwamba hayo mabomu kutoka Burundi yakishafika yatachagua baina ya Muunguja na Mpemba? Au hata Mtanganyika? Serikali inafanya nini juu ya waraka kama huu? Tuseme hawaujui? Hawajaupata? Waziri wa nchi yuko wapi aje hapa tuhangaike naye? Kamishna wa polisi yuko wapi aje hapa tuhangaike naye? Na huyo naye Nchimbi yuko wapi aje hapa tuhangaike naye?

Kwa kumalizia narejea suala langu la kwanza: Haiwi kuwa kupenya kwa waraka huu ukawa ni sababu ya mauwaji yanayotokea hivi sasa Zanzibar? Ndugu zangu tusaidiane fikra katika maoni yenu juu ya mada hii.

Share: