ZenjiLikiz

TETEZI:MEMBE AKALIA 200BN/= ZA ZANZIBAR

Kumbe zipo sababu nyingi kuwasikia wajumbe wetu wa BLW wanasema kwa ukali, ghazab na jazba wanapozungumzia haki ya Zanzibar ndani ya Muungano; dhulma inayofanyiwa Zanzibar ndani ya Muungano – na kelele zinapokuwa nyingi, zinaundwa kamati. Mpaka sasa zimeundwa kamati 200 kutatua kero (KARO) za Muungano; karo hazijasafika.

Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na “Ushirikiano wa Kimataifa” amekalia pesa za Zanzibar zipatazo 200bn/= zilizotolewa na wafadhili kwa ajili ya kuipa Zanzibar kuendeleza/kufufua specifically zile EPZ, maeneo huru ya kiuchumi Zanzibar.

Waliotoa pesa hizi wakiwemo UAE/Rasil Khemah – ambao viongozi wetu wote watatu (Shein, Seif-1 na Seif-2) wamekuwa kiguu na njia kutafuta misaada. Imepatikana Membe – laatul laah amezuia, just kutia saini tu ili pesa ziwe released.

Kipengelea kimoja kinachomfanya Membe ndiye atiwe saini/pesa za misaada, mikopo, zawadi n.k zinapoingia katika foreign currency au misaada kama hiyo – Zanzibar hairuhusiwi kusaini, kwa sababu ‘si nchi’ inatakaiwa TZ ndio imwage wino.

Huu ni mwezi wa pili, Membe amekalia barua yetu na pesa zetu, halali yetu. Baadaye wanakuja Zanzibar eti kujiliza baada ya meli kuzama.

Hiyo ndio TZ, na huo ndio Muungano wetu uliodumu miaka 48 kwa Bara kuidhulumu Zanzibar.
* Plus, jana tu Abubakar alikuwa anasema ndani ya BLW kuwa hao hao akina Membe wameinyima Zanzibar fursa ya kuhudhuria vikao muhimu vya kimataifa kwa kuwanyima wajumbe wake visa, just kwa sababu wao watanganyika hawakwenda au hawakutakiwa kuwemo.

Ushauri wangu: MAMBO YA NCHI Z ANJE IONDOSHWE KABISA KATIKA LIST YA MUUNGANO (GET ME RIGHT PLEASE, SIO SUALA LA KUGAWANA MABALOZI, LA HASHA). ONDOA FOREIGN AFFAIRS KATIKA LIST HIYO FOR GOOD.

Mbaya zaiid katika sakata hili la Membe kuzuia pesa zetu, naibu wake anaitwa Mahadhi Juma Maalim – mzanzibari wa Muyuni/na Mungoni (huyu ni kambi ya NO vote katika referendum, na ndiye group la akina Samia, Haroun, Shamsi, Perera Ame Silima – wanachochea watu wa kusini wasema NO serikali tatu au muungano wa mkataba). Mahadhi, Kazi ya uzinzi haifai na kutafuta wanawake kuowa. Kuwa na akili wewe, nchi yako inazamishwa.

Hizi habari za Membe kukalia 200bn/= zimeigusa BLW na cabinet ya Zanzibar – ni habari zilizoleta ghazab sana, maana hili si la mwaka 1968 au 1980s au 1970s – it’s only two months ago or less (jana na leo).

Naomba wana-mzalendo tujadili mada hii kwa kina na tuone impact yake. La kama mtaona abdisalum porojo – sawa. Maana huko nyuma nilisema mengi – mkaona ahhhh….huyu haipendi CCM + CUF na haitakai GNU tu. Leo akina Moyo, Jussa, Hamza, Mansour – wanasema hayo hayo niliyosema mimi long time ago.

Mfano niliwahi kusema katika ukumbi huu kuwa ‘ushirikiano wa kimataifa’ limeingizwa baada ya zahma ya Zanzibar kutaka kujiunga na OIC; awali ilikuwa haimo. Mzalendo walipinga baadhi yao – juzi Moyo amelisema, na ameonekana ‘champion/hero’.

Hii ya membe sijui kama haitopingwa, lakini ulizeni wana-cabinet wa SMZ , muulizeni Mahadhi na huyo bosi wake Membe – kweli si kweli?

Kidumu Chama Cha Mapinduzi – Udumu Muungano wa Serikali Mbili kuelekea MOJA TUUUU….!

Tagsslider
Share: