ZenjiLikiz

Msafara wa Lowasa wazuiwa msibani

11838638_766736250104018_3189640585422974703_o

11822644_827287600721233_2620922360165982130_n
Polisi wa Mwanga mkoani Kilimanjaro wamezuia msafara wa Edward Lowassa kijiji cha Maroro Wilayani Mwanga sasa hivi akiwa ameongozana Mbatia, Ndesamburo na Augustino Mrema ukielekea msibani kwa madai kuwa wanaosindikiza msibani ni wengi sana.

Msafara wa Lowassa wazuiliwa na Polisi wakati msafara wake ukielekea kwenye mazishi ya Peter Kisumo.

11856528_766736266770683_4263750936932267814_o
Leo ni siku ya mazishi ya mzee Peter Abdallah Kisumo ambae ni mwasisi na ameshika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwaziri, ukuu wa mikoa na uenyekiti wa mashirika mbalimbali ya umma na mazishi yanatarajiwa kufanyika kijijini kwao Usangi katika wilaya ya Mwanga katika makaburi ya familia.

Kisumo aliaga dunia Agosti 3, 2015, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, ambako alikuwa anapatiwa matibabu ya figo, ikiwa ni mwezi mmoja tangu arejee nchini akitokea nchini India.

(HABARI HAINA UTHIBITISHO ZAIDI YA PICHA -TUTAJUA BAADAE -KUTOKA ZANZIBAR HUMAN RIGHTS FACEBOOK) TUMEIWEKA WIKILIK MAKUSUDI HADI BAADAE

Share: