ZenjiLikiz

Ujumbe wa wazee Pemba kwa Maalim Seif

unnamed (45)
Katika kikao cha ndani cha Wazee wenye nguvu na wenye kuheshimika kwa Pemba mzima wametuma ujumbe wao kwa Maalim Seif Shariff Hamadi kua arudi haraka kisiwani Pemba Mara moja pindipo akipata Ujumbe huo ili wende wakamtawazishe kuwa Rais wa Watu wa Zanzibar kwa kwa vile yeye ndio raisi mtarajiwa na kinachosubiriwa kwa sasa ni kutangaziwa tu.

Katika maelezo yao wzee hao wamesema ikiwa Serekali ya Smz na ile ya Smt wameweka mkwamo huo wa kuto kuteua mwenyekiti mwengine ili aendelee kutoa takuimu na hatimai kupata raisi Zanzibar ambae kwa mujibu wa takuimu za Zanzibar mzima na uchahidi ulopo nikua Maalim Seif Shariff Hamadi ndie Raisi anae subiri kuapishwa .

Katika tamko lao Wzee hao wa kisiwa cha Pemba wamesema kazi hio wataifanya wao pindipo Raisi mtarajiwa Maalim Seif Shariff Hamadi atakubali kuitikia weto wao na kurudi Pemba mara moja kwa Kwenda kutawazisha kuwa Raisi wa Watu wa Zanzibar.

Wamesema hivi sasa shwala hilo limewekewa mgwamo na viongozii wakuu wa ccm akiwemo Dr Shein na Mh Kikwete kwa kuona jaribio lao limefeli lakutaka kufanya ubadhirifu wa kuwaibia Wzanzibar haki yao ya kidemocrasia kumshagua mtu ambae sio chaguolao Dr Ali Muhammed .

Kutokana na ushahidi tosha kua Maalim Seif ndio chaguo la Wananchi wa Zanzibar Wazee hao waliomua kukusanyana na kutoa pendekezo lao hilo na baadae kutuma ujumbe mzito kwa Maalim SeifF ili arudi kisiwani Pemba wente wakamuapishe kuwa Raisi wa watu wa Zanzibar pindipo Maalim atawakubalia ombi lao hilo na kurejea Pemba kwa Kazi hio.

Wazee hao Walitoa tamko lao hilo juzi na Mpaka sasa katika maelezo na wazee hao wanasema bado Maalim Seif Kashindwa kuwapa jibu la kiuhakika na wametuma ujumbe wao wa Mwisho wakumwambia pindipo akiwa kimya na kushindwa kuwajibu au kuwapa maelezo ya kina basi wao watajikusanya na Kwenda UN kudai nchi yao ya Zanzibar Full Sovereignty .

Wamesema kwa hali ilivyo sasa Zanzibar nikua Raisi wa Tanzania Jakanya Mrisho Kikwete imekua anaonyesha uhuni kutokana na kuzarau na kutupilia mbali madai ya Wananchi wa Zanzibar kwa mujibu wa Sheria ya Zanzibar ya 1984.

Wzee hao katika maelezo yao wanasema Zanzibar ni nchi inayo fuata sheria na kanunu za nchi yake na ina katiba yake yenye kuheshimika lakini imekua kama vile haiheshimiwi na Serekali ya Muungano SMT na kufanya watakavyo kwa nguvu za utashi wa kichama, wzee hao wamefika mbali kusema ulimwengu wote unafahamu kua zanzibar ina utawala wake wa ndani na Sheria yake na katiba yake.

Kwa hio basi wao watakwenda kudai haki ya Wananchi wake katika misingi ya kisheria na kidemocrasia , Wzee hao wameshangazwa na Serekali ijitayo ya Muungano kutumia kura za wapiga kura wa Zanzibar kama sehemu ya Muungano na kumuhalalishia Mh John Pombe Makufuli kua Raisi na huku wakichukua kura halali za Wananchi wa Zanzibar kuzifuta na kuzarau haki na democrasia ya wapiga kura wa Zanzibar.

Hiiwamesema ni kitendo cha kihuni alisho wafanyia Kikwete na hakina mashiko yoyote yakisheria kwa vile wazanzibar walikisha piga kura katika vituo vyote vya Unguja na Pemba na kura zilikwisha isabiwa na takribani majibo yote ya Unguja yalikwisha tangaziwa majimbo 31 .

Vipi leo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jesha Salim Jecha kwa Utashi wake wa ukereketwa na sindikiza la chama chake kutufanyia mambo haya ya kihuni na yasio na mashiko yakisheria ?

Kwahio Wazee hao kutoka Pemba wametoa tamko la pamoja na kusema watashirikiana na wazee wenzao wa Unguja ili kuenda United Nation offisi yao na kupeleka malalamiko yao kudai Full Sovereignty ya Zanzibar kwa faida ya vizazi vyao vya sasa na vijukuu vyao vijavyo.

Wanasema wameshoshwa na kuona kila ufikapo uchaguzi mkuu wananchi wa Zanzibar wasio na hatia yoyote wanamiminiwa Jeshi la JWT mitaani katika makaazi ya raia wa Zanzibar na kuwatesa na kuwafanya waishi kwa hofu huku wakishingizia viashirio mbali mbali vya uongo ikiwemo kutangazia hali ya hatari ya mambomu kutegwa.

Share: