ZenjiLikiz

Tetezi:ZEC kupangua majimbo visiwani Zanzibar

Taarifa zilizonijia hivi punde kutoa vyanzo vyangu vya Habari Tume ya Uchaguzi Zanzibar imefikia hatua ya kuyakata majimbo 2 ya Uchaguzi kule kisiwani Pemba ili kukamilisha adhma yao ya kufanya hila katika uchaguzi Mkuu ujao kwa upande wa Zanzibar. Pemba Jimbo la Mgogoni na Jimbo la Chonga Wilaya ya Chake.

Jimbo la Mji mkongwe ambalo kwa sasa Mh Jussa ndio mwakilishi pia limefutwa kuongezewa Kikwajuni na Pia Jimbo la Fuoni kufanywa majimbo 2 badala 1. Kwa hiyo sasa Unguja kutakuwa na majimbo mengi Zaidi ya Uchaguzi na Pemba kupunguzwa.

Ikumbukwe kwamba hali hii imekuja katika mikakati ya CCM kuhakikisha CCM inashinda tena Uchaguzi Zanzibar wakiwa na matumaini kwamba Unguja CUF haina nguvu kwa hivyo majimbo yakiwa mengi kwa Unguja ni mpango mzuri kwa CCM.

Taarifa hiizi mkali wangu ameniambia huenda ikatangazwa soon kuanzia leo saa 9 za mchana na Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

Naomba kuwasilisha.

chanzo:JF

P:S
**Habari si rasmi kama inavyosema si habari rasmi – ni vidokezo tuu hivo.Habari rasmi hadi itangazwe na vyombo husika

Share: