ZenjiLikiz

TUME YA KATIBA YATOA RASIMU YA AWALI

  •  MZALENDO.NET haijaweza kuithibitisha habari hii.Hivyo imerudishwa kama ni tetezi (habari zisizo rasmi), na msomaji anaombwa kuwa hadhari.

Breaking News

HATIMAYE Tume ya Mabadiliko ya Katiba, imekamilisha mwelekeo wa Katiba mpya, na kupendekeza mfumo wa Muungano wa Serikali mbili au tatu.

Hii ni kwa mujibu wa rasimu ya Katiba inayotarajiwa kutoka Jumatatu Aprili 8, mwaka huu kabla ya kujadiliwa na wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.

Taarifa za uchunguzi kutoka ndani za Tume, zimesema Makamishna wa Tume hiyo wamefikia muafaka wa mapendekezo hayo, baada ya uchambuzi mkubwa wa maoni ya wananchi kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Rasimu ya Katiba hiyo, inatarajiwa kufikishwa katika Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, ambayo wajumbe wake waliteuliwa hivi karibuni katika shehia mbalimbali.

Wajumbe wa wilaya ya Mabaraza ya Katiba, wanatakiwa kufanya uchambuzi wa maoni, kupitia mwelekeo wa rasimu hiyo na hatimaye kuirejesha tena kwa Tume ya marekebisho ya Katiba mpya.

Muungano wa Tanzania, wa Tanganyika na Zanzibar umekuwa katika mfumo wa Serikali mbili tangu ulipoasisiwa, Aprili 26, 1964.

Hata hivyo: Historia inaweza kubadilika endapo turufu mbili zilizopendekezwa na Tume ya Katiba, moja itashinda, hasa mfumo mpya wa serikali tatu.

Aidha, habari zaidi zinafahamisha kuwa Tume hiyo, imetupilia mbali maoni ya Muungano wa MKATABA..

Tagsslider
Share: