Habari

Ziara ya Maalim Seif Nchini Qatar na mafanikio yake

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amewasili Zanzibar salama usalimini na amepata nafasi ya kuzungumza na Waandishi wa habari.

Amesema alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar alimwambia waziwazi kwamba wananchi wa kawaida wa Qatar hawaijui Tanzania lakini wengi wanaijua Zanzibar kutokana na mahusiano ya kihistoria yaliyopo baina ya nchi mbili hizi.

Maeneo waliyokubaliana kushirikiana ni pamoja na:

1. Qatar kuangalia uwezekano wa kuijengea Zanzibar Environment Resource Centre ili kukabiliana na athari za mazingira.

2. Qatar kuisaidia Zanzibar kuanzisha mfumo wake wa kuzalisha umeme wake wenyewe.

3. Qatar kuisaidia Zanzibar katika mradi wa kumaliza tatizo la maji khasa Mkoa wa Mjini Magharibi.

4. Qatar kuipatia lami Zanzibar kiasi cha tani 10,000 kwa ajili ya matengenezo ya barabara.

5. Qatar kuangalia jinsi ya kuwekeza katika uendelezaji wa Uwanja wa Ndege Pemba ili uweze kutoa huduma za kimataifa.

6. Qatar kuangalia namna ya kuwekeza Zanzibar katika Ujenzi wa Bandari maalum ya kushughulikia utoaji wa huduma kwa sekta ya mafuta na gesi asilia.

7. Qatar kusaidia Zanzibar katika kuendeleza Karume Institute of Science and Technology na Kengeja Technical Secondary School kuwa za kisasa.

8. Qatar kuona uwezekano wa kusaidia madrasa za Zanzibar kwa kuziimarisha na kuzipatia vifaa.

9. Qatar kuwapatia ajira vijana wa Zanzibar lakini kwanza kwa kuanzisha vituo hapa hapa Zanzibar vya kuwapa mafunzo ya aina za kazi wanazoweza kuifanyia Qatar.

10. Qatar Investment Authority na Qatar Development Fund kuleta ujumbe Zanzibar kuona maeneo wanayoweza kuwekeza na kufanya kazi kwa pamoja na Zanzibar.

Amesema kinachofuata sasa ni ufuatiliaji na kuchukua hatua madhubuti kuyafanikisha haya.
Chanzo: Ukurasa wa Facebook akaunti ya Mh. Jussa

Tagsslider
Share: