Habari

ZINDUKA: Damu ya Tundu Lissu, Iwe Ngao ya Mapambano:

Napenda kuchukua fursa hii adhimu kupeleka  Sala na Dua zetu kwa Mh. Tundu Lissu ambae amepigwa risasi  na watu  (Ati) wasiojulikana  huko nyumbani Kwake Dodoma. Kabla yakuanza kuandika shutuma zangu kwa wahusika wakuu wa serikali ya CCM, napenda kuwaomba Watanganyika na Wazanzibari wote wanaopenda kuona utawala Bora na Democracy ya kweli, kulaani vikali kitendo hichi cha kidhalimu alichofanyiwa nduguyetu Mh. Tundu Lissu. Na ikiwezekana Kufanya Maandamano hata kama hakutakuwa na Kibali. Tukumbuke maandamano ya Amani ni haki ya kila Raia kuonyesha feellings zake.

Pili ningeomba kila Mtanganyika na Mzanzibari au hata wa East Africa kumuombea dua kiongozi wetu/ ndugu yetu mzalendo Mh. Tundu Lissu katika sala zetu- ili Allah (SW) ampe afya yake haraka na aungane na sisi katika kupigania Haki na Democracy ilioporwa na Utawala huu dhalimu wa CCM.

Leo nitapendelea kuihusisha Makala hii  na vipengele 3 vifuatavo hapo Chini ambavo kwa mtizamo wangu naona ni vitu vyakuvichambua.

  1. Wataalamu wa Psycology husema:  Adui huwa wa mwanzo kutoa masikitiko yake juu ya tukio:
  2.  Tuichambue kwa makini kauli ya Humphrey Polepole miezi 3-4 iliopita, Ilikuwa na maana gani?
  3. Damu Zao  ndio ngao za kuondowa utawala dhalimu wa CCM Tanganyika na Zanzibar

1. wataalamu wa  Psycology  adui huwa wa mwanzo kutoa masikitiko yake juu ya tukio:

Kutokana na wataalamu wanaochunguza case za jinai au genocide  (matokeo ya uhalifu) wanasema kwamba mtu wa mwanzo ambae ataonyesha  hisia zake/imani  au kisikitishwa na kitendo cha Uhalifu/ Mauwaji basi huyo nilazima awekwe kuwa kama ” Primary Suspect” Hivi ndivo nchi nyingi duniani wanavofanya  investigation zao wakati wakuchukunguza matukio ya case za genoside/ uhalifu. Na hutokea ikawa huyo promary suspect ndie anaehusika na mauwaji au plan ya mauwaji au uhalifu huo. Lakini hii inatakiwa kuwe na polisi waliokuwa wamebobea kwenye masuali ya uhalifu, wawe wanajua na kuheshimu sheria za nchi na tatu wawe wako Indipendent na sio kukubali kutumiliwa na kundi fulani au chama fulani.

Hivo nina uhakika wa 100% kwamba kwa Upande wa Tanganyika na Zanzibar hatuna polisi Investigation yoyote itakayoweza kulichunguza suali la Mh. Tundu lissu bila yakupita Mkono wa CCM ambao utazuia Ukweli.  Hii nikutokana nakwamba Polisi na vyombo vyote vya Dola Vinatumiwa na Serikali tawala na Chama cha CCM.  Mifano tunayo mingi ya Matokeo ya Kihalifu ambayo yametendwa kwa wana siasa wakongwe na wa sasa. Na mpaka sasa tunasubiri majibu ya watu waliouliwa au kupotea bila hata ya Tress. Mfano ni akina Ben Saanane na viongozi wengine waliouliwa kule Zanzibar wakati wa 1970s. Na ndio maana tumeshaambiwa  kabisa Mh. Tundu Lissu amepigwa Risasi na Watu Wasiojulikana. Itakuwaje Taifa liwe na Uchawa chawa wa Jeshi na Polisi halafu raia wake wawe wanatekwa wakiuliwa ovyo ovyo, kutolewa pistol hadharani na kupigwa risasi na vyombo vya habari vifanye kigugumizi kwakusema wahalifu wa CCM na john Pombe ni Watu Wasijulikana?

Sisi Wazanzibari tunajuwa hao watu Wasiojulikana ni Mazombi ambao huitwa “USALAMA wa TAIFA”  ambao wanaitumikia Serikali ya CCm. na napenda kuweka wazi kwamba, kwa Vyombo vya Habari vya Kitanganyika na hata kule kwa Wale Mzumbu kuku kule Zanzibar. Naamini hakuna Chombo cha habari hata kimoja kitakacho thubutu au kuja na Consperacy Theiries of Medialogy. Hii nikutokana nakutokuwa na Independent Medialogy- vyombo vyote vya habari  vinaogopa. Hasa kwavile kushawahi kutokea uvamizi  wa kishenzi na kutishiwa silaha  kwa waandishi wa habari wa private media.  Na kwa upande wa Zanzibar vyombo hivo vimechomwa Moto na kusababisha hata ulemavu wa watangazaji… Hapa ndipo Chama hichi cha CHristian Movement Crusaid (CCM) ndipo kilipotufikisha na wako tayari kuiona Tanganyika na Zanzibar inakuwa kama Ruwanda lakini wao waendelee kututawala na Vitukuu vyao.

 

Ninavojuwa mimi Usalam wa taifa wanatakiwa wa react wakati Nchi inapokuwa inahatarishwa na Wageni au watu wanaotumiliwa na wageni kudhoofisha Uchumi na maendeleo ya jamii. Usalam wa Taifa wanatakiwa wawe Invigilant wakati Raisi au kiongozi yoyote wa wananchi anaponyanyaswa na si vyenginevo.  Usalama wa Taifa wanatakiwa wawe INDEPENDENT na NUTRAL na SIO Kukitumikia Chama  cha CCM  na Kuikandamiza haki za  wananchi Wanyonge amabo huchagua viongozi wao ili wawatumikie.Kama tuna independent Police Force wanaoshuhulika na matokeo ya Uhalifu hasa wa attempted murder basi wangeanza kuchunguza mwenondo tokeo la upoteaji la Ben saanane, uporaji wa madaraka halali ya Wazanzibari na matukio yakuchomwa Moto kwa TLS au kupigwa risasi kwa Mh. Tundu Lissu.

 

Nikirudia kwenye Makala yetu, kitendo cha John Pombe (Mtukufu Mfalme)  na Kibaraka wake Humpherey polepole- kutoa masikitiko yao au kuwa wa mwanzo kujifanya wanasikitishwa na kitendo hiki. Huku wakinyamazia matokeo mengine makubwa ya Uhalifu wa kutumia Silaha za Moto. Kunanifanya moja kwa moja niwa suspect hawa ndio Master Plann wa shooting.  Ndugu Watanzania wa Zanzibar na Tanganyika, wakati umefika wakuamka na kuacha woga, kitendo cha Unyanyasaji wa Viongozi ambao ni Watetezi wa Utawala Bora tukikiangalia Pembeni basi hakuna atakaekuwa Salama.

2. Tuichambue kwa makini kauli ya Humphrey Polepole miezi 3-4 iliopita, ilikuwa na maana gani?

Nduguzangu wa Tanganyika na Zanzibar, kama mutakumbuka miezi 3-4 iliopita, Humphrey polepole ambae ni Katibu muenezi wa CCM NEC aliwahi kuhojiwa na na Sauti ya Ujerumani, Idhaa ya Kiswahili- iliorushwa na nduguyetu Mohammed Ghassani kuhusiana na uimarishaji wa CCm. Mtangazaji huyo wa Dochiveli pia aliwahi kumuuliza suali la mgogoro wa Zanzibar lakini Humphrey hakutaka kusema nini kitatokea. Nakumbuka niliwahi kurushiwa audio ya mahojiano hayo katika Social Media. Nini Humphrey alisema? Namnukuu hapo chini ( lakini kama nitakuwa nimesahau basi mutanirekebisha):-

” Tunataka Ngojeeni katika miezi mitatu hii ijayo, Watanzania watashuhudia mambo makubwa sana yatakayo tokea…” Mwisho wa kumnukuu

Kwa upande wangu nilipomsikia Polepole  akisema kuhusu mambo makubwa yatakayotokea Tanzania ambayo yatawashituwa Watanzania nilijuwa hakuna utawala wa Haki wala democracy Tanzania. Na Suali la Zanzibar nilijuwa Humphrey ni Aduwi Mkubwa wa Wazanzibari kama alivokuwa Nyerere na Samuel Sitta au LUKUVI. Matokeo hayo alioyasema Humphrey Polepole ni:

a. Kumtumia Lipumba kuichafua CUF.

b. Kuvitumia Vyombo vya Dola kuwakandamiza Wapinzani na Democracy Tanzania.

c. kuwatisha Wapinzani na hatimae kuwapiga Risasi kama tukio hilo la Mh. Tundu Lissu.

Hayo ndio mambo 3 makubwa yaliotushituwa Watanzania katika miezi 3-4 aliosema Humphrey Polepole kama yangetokea. Ukweli nikwamba utawala wa CCM ni utawala wa KIDICTATOR na hauna tofauti na ule wa General Pinachaet wa Agentina au Cambodia. Hakuna njia mbadala ya Haki au democracy kusimama hapa Tanzania. Na tukio hilo alilofanyiwa Mh. Tundu Lissu ni Wake Up Call kwa Majaji wa Mahakama kuu wanaoshuhulikia Case za CUF.

Jee kitendo hichi kitaweza Kuzuia Nguvu ya Watanzania kudai utawala Bora na Democrasia ya kweli?

Au tutaendelea kutoa macho nakuogopa? Time will Tell.

3.Damu Zao  ndio ngao za kuondowa utawala dhalimu wa CCM Tanganyika na Zanzibar

Tumeweza kuona Nchi nyingi ziliokuwa zinapigania haki, democracy na hata uhuru wao basi zilipoteza damu. Labda Nchi ya TANGANYIKA ndio Iliopigania UHURU bila yakumwaga Damu. Nashangaa sasaivi Utawala wake wa CCM unatumia Damu za nduguzetu Wazalendo kueendelea kututawala. Mfano ni Yale Mauwaji aliofanya Benjamin MKapa kule Pemba 2001. Na viongozi mbali mbali waliotekwa nyara na kupotea, hizo ni Damu za nduguzetu Wazalendo wanaodai Utawala Bora.

Kwa Upande wa Zanzibar tumeweza kuona kwamba Mauwaji yaliofanyika Pemba na Ukandamizaji wa Wazanzibari ndio imekuwa CHACHU yakuiondowa CCM kule Zanzibar. Tumeshuhudia katika Uchaguzi wa 25.October 2015 na ule Uchaguzi wa CCM-Mazombi 16.March 2016. CCM Tanganyika Waliweza kuona kwamba Hawana watu Visiwani kwani Nguvu ya Upinzani imezidi baada ya kumwaga Damu zao na ukandamizaji. Hivi sasa Chama hicho Kinatumia JESHI na Watu kutoka Nchi za Africa au Tanganyika kuwapigia kura.

Jee Watanganyika Wanaweza kufanya Mageuzi kama yaliofanywa na Wazanzibari?

Nilikuwa nawaomba nduguzetu wa Tanganyika ambao wanaamini Utawala Bora na Wenye Democrasia ya kweli kukichukulia kitendo hichi kama CHACHu ya Mapambano na hatimaye kuiondoa CCM. Tukumbuke Waswahili Wanasema ” Tumbiri akikosa Miti, Basi Huingia Muilini”

Na Serikali ya CCM imekosa Sera, Utawala Bora wakuwafanya Watanzania hasa Wazanzibari Waichague, sasa wanatumia Nguvu na vitisho kuendelea Kututawala Wao na vizazi vyuao vijavyo. Kwani Kila kiongozi wa CCM sasaivi anakula na Family yake. Mifano tunayo. Hakuna kiongozi wa CCM aliekuwa hana Mtoto au Mjukuu JUVI-CCM, Mbunge, Waziri, Mkuu wa Usalam. Ni Utawal a wa KIFALME wanarithishana.

Share: