Habari

Zomea zomea ilioanza Visiwani Z’Bar zidi ya wasaliti, Jana ilimkumba Mwakilishi wa Koani Mussa Ali Hassan

Kulia ni Muwakilishi wa Koani Mussa Ali Hassan

Zomea Zomea jana imemkuta Mwakilishi wa Koani. Mussa Ali Hassan hapo katika Soko la Mboga Mboga kwa Mchina Mombasa, kiasi cha kuhumiwa na kupanda Taxi kwa fedheha na Kuliwacha gari lake alilo kwenda nalo hapo Sokoni. Msaliti huyoo…. dalali huyoo…,, msaka tonge huyoo…… mnafiki huyooo…., huyoo …. huyooo .. wewe si ulisema UKAWA Waondoke kabla hujarudi wewe….. Utaondoka wewe Fisadi wa Mafisadii hayo ndio yaliomkuta fisadi Mussa Ali Hassan, na kuhemewa kama vile kuku mgeni mwenye kuhemewa.
Hali hii imewakumba badhi ya Wabunge ,Wawakilishi na Wajumbe wa Tasisi mbali mbali kutoka Zanzibar.
Wananchi wa Zanzibar wamechukua msimamo huo wa kuwazomea na kuwatupia maneno ya kua ni wasaliti wa Zanzibar wenye kuiuza Zanzibar kwa kusaka Tonge za Matumbo yao.

Mambo hayo yamekua yakitokea sehemu tafauti za Mji wa Zanzibar pale wapitapo na huzomewa na kurushiwa maneno hayo, Jana ndio yalimkumba Muwakilishi wa Koan Mussa Ali Hassan Zidi ya wananchi wa Zanzibar wenye hasira.

Share: