Habari

Zuluma za CCM tiliona ni sawa kwa Wazanzibari, Sasa Wafanyiwa Watanganyika

Makala ya 1

By James Mapunda

Habari za mchana huu ndugu zangu wa ndani na nje ya Zanzibar na Tanganyika. Balaka na amani za Ijumaa ziwafikie ware ndugu zangu Waisilamu. Leo nimekuja na mada yakuwazindua ndugu zangu wa Tanganyika ambo wanaendelea kudanganywa danganywa na John Pombe Magufuli na inner Circule yake ya utawala wa CCM awamu ya 5. Nitapenda kuzungumzia mada tatu ndefu ambazo nitachambua uongo wa Selikali ya  maraika na upigaji vita wa RUSHWA na UFISADI.

Kabla sijaenda mbere, napenda kuwakumbusha ndugu zangu Watanganyika, wapenda kusoma Historia ya Muungano wetu ambao ulinyanganya madalaka ya “Zanzibar Government na Kuyaweka kwenye  Tannganyikans Government. 26.April 1964 , miezi 3 tu baada ya Mapinduzi ya Zanzibar. Katika kipindi cha miaka 40 chote, Watanganyika wengi turikuwa tukiona  (hata mimi) wazanzibali wana lalama sana pare waliposema Muungano unawanyonya na kuwazurumu haki zao kama Nchi  ilio huru. Sasa  miaka 56 imepita ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na tumeweza kuona kure Zanzibar hakuna tena kitu cha kuzurumiwa. Kwasababu Wazanzibari wmewekwa kwenye Magonvi ya kindugu na Kubaguwana na Zanzibar imekauka.

My point is now The Tanganyikans Government under Magufuli and CCM party bergun to Decapitate Tanganyikans peoples, its economy and its national resourcess. Na hii nikutokana na kuwa na Katiba Mbovu ambayo imempa Mamlaka makubwa Raisi wa Muungano kufanya anavotaka. Hata tumeona kwamba Raisi anaweza kuamua nani ana haki ya kufa na nani ana haki ya kuishi iseee… Naamini kuna nduguzangu wa CCM hasa ware waliopewa madalaka makubwa au kupandishwa vyeo vikubwa hawata nifahamu. Lakini nataka kuwaonyesheni mifano ya  kwanini nasema Selikali ya CCM Tanganyika sasa inawazurumu hata WatanganyikRushwa na Ufisadi:

1.Uuunjifu wa Katiba na Sheria za Nchi:

Serikali ya Magufuli 2017 ilitwambia kwenye Front line za Magazeti kwamba  Serikali inaa idai  kampuni ya Madini ( BAREC) §§§  zipatazo billioni 194 ambazo ukiziweka katika TSh ni sawa na  more than 400 Trillions Shillings. Juzi tena walisahau kama ripoti yao ya mwanzo ipo wanakuja na repoti yakusema kwamba hela tunazotaka kulipwa na Barec ni 300Million. Hizo hela nyengine zimepoterea wapi?

Tafadharini tumuulize Magufuli na Chama chake hio hela nyengine ya difference wameipeleka wapi? na hio US § 300millioni iko wapi na itafanyiwa kazi vipi?

2. Uvinjifu wa Bunge ambalo ndio Chombo cha Kutunga Sheria na Bugeti za Matumizi:

Nduguzangu Watanganyika na Wazanzibari tumeweza kuona ni jinsi gani Serikali ya CCM kupitia Raisi Magufuli anavoingilia kati mihimili ya Bunge katika Budgeti zake.  Kutokana na repoti ya CAG mzibiti na Mkaguzi wa hela za Serikali, amesema katika repoti yake kwamba kuna hela Trillioni 2.4 hazijulikani zilikokwenda na CAG alipoulizwa aliambiwa na Job Ndugai kwamba ataitwa kwa Pingu. Na hapa nduguzangu Watanganyika tutaweza kuludisha kumbukumbu sababu za Magufuli kukataa Bunge lisioneshwe Live. Ni hizi za Bunge zakupitisha Budgeti yake Kisha Raisi akaifumua fumua na kufanya anavotaka yeye. Mwaka 2013 na 2014 katika Utawala wa Kikwete Kulipotea Hela Trillioni 3. kwa Scandal ya ESCROW ambazo akina Tibainjuka, Chenge na Mawaziri wengine Wa Tanganyika waligawana.

Mfano wa Budgeti ya Ofisi ya Raisi ilikuwa ni Millioni 100 kwa matumizi ya mwaka 2016-17, lakini Magufuli aliifumua nakuzidisha budgeti hio mala 5x. Alafu mtu huyu huyu anasema yeye ni Laisi wa Malaika na Wanyonge na anapigana na ufisadi na Wala Rushwa. Kwa Muono wa Watanganyika walio na akili tunaweza kuona kwamba Magufuli amepunguza tuu Idadi ya Wala Rushwa na sio kuzuia Rushwa. Sasa Rushwa na Ufisadi Unatafunwa na kugawanywa na  ” The Inner Circile ya Magufuli na UV CCM ambao wako tayari Kunywa damu za Wapinzani au Kuharibu mali za Wananchi.

3. Kuwanyanyasa Wakulima:

Wakulima Wa Korosho waliambiwa na Magufuli kwamba Soko la Korosho ni Serikali yake na watazibagua na kuuza Korosho Safi. Wakulima wengi walifurahia jambo hilo na wakaapeleka Korosho zao zenye Viwango vizuri kwenye Soko la ndani. Hatimaye tumeona Korosho za Wakulima zililundikana hadi zimeanza kuota miche. Hii inaonyesha kwamba Selikali ya Magufuli haikuwa na hela yakulipa au Utaalamu wakuweza kubagua korosho, hatimae wakulima wanaanza kuludishiwa Korosho zao na kuambiwa hazina Viwango. Wakati Ni serikali ya CCM ndio imezushusha viwango Korosho za Wakulima kwakuziweka katika Magala kwa muda mlefu. Chakusikitisha zaidi Wakulima hao walikuwa wameingia katika mikopo tofauti kwakutegemea kupata hela zao Serikalini. Lakini hakuna kitu hadi sasa. Harafu Magufuli anasema yeye ni Raisi wa wanyonge..Isee. Ni wanyonge gani sasa hao au wale MA Kada wenu munao wanunua kule Vijijini?

Serikali ya CCM imekuwa ikijiingiza katika Biashara ya Korosho, kuwakandamiza Wabunge wa Wananchi ambao wanatoka upinzani na kuwafukuza katika majengo ya Serikali au kuwapandishia kodi kubwa kupita kiasi -wakati wabunge hawa wanawatumikia Wananchi katika majimbo yao. Huu Ndio Utawala Wazanzibari wameukemea kwa miaka mingi na tukiwaona Wana lalama kila siku. Lakini sasa haya yanatufika sisi Watanganyika na tunayachekelea au kutumia vyombo vyetu vya habari kuyapa baraka zote.

Inaendelea : Usikose Kusoma Makala ya 2

 

 

 

Share: