Makala/Tahariri

CCM na Jecha toweni ushahidi wenu (vielelezo) hadharani!

Kwa ufupi:

CCM na Jecha toweni ushahidi wenu (vielelezo) hadharani msicheze na akili za watu.

Mwandishi Maalum,

Ni zaidi ya mwenzi mmoja tokea CCM na tume yake ya uchaguzi ZEC (Jecha) walipoamua kufuta matokeo yote ya uchaguzi ulio fanyika tarehe 25 Oct 2015 baada ya kuona CCM imeshindwa vibaya.

Tukio hilo la aibu lilikuja kufuatia kikao kilicho washirikisha Jecha Salim Jecha (Mwenyekiti wa ZEC), Salum Kassim (Mkurugenzi wa ZEC), Naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na makada wenzake wa CCM.

Baada ya majadiliano ya muda mrefu ikaonekana hakuna njia yoyote itakayo weza kuinusuru CCM isipokuwa kufuta uchaguzi, jambo abalo liliungwa mkono moja kwa moja na viongozi wa juu wa CCM Tanganyika.

Kituko ni pale Nd. Jecha alipo jitokeza kwenye video iliyo rekodiwa na ZBC akitoa tangazo la kufuta uchaguzi bila kutaja kifungu chochote kinacho mruhusu kufanya hivyo, huku akitoa sababu zisizo kuwa na mashiko. Baada ya wanasheria kulalamikia uvunjwaji huo wa sheria, ghafla tukaona maigizo katika gazeti la serikali likitoa maelezo yaliyokuwa tofauti na ya Nd. Jecha ambapo gazeti lilinukuu vufungu wakati katika taarifa ya Nd.Jecha iliyotolewa kwa njia ya video hakuna sehemu anayo nukuu kifungu chochote cha sheria.

Tunawaomba CCM watueleze ni ipi sahihi kati ya taarifa hizi mbili, taarifa ya Jecha kupitia video au taarifa Ya Tume(Jecha) kupitia gazeti la Serikali.

Tumesikia malalamiko mengi kutoka CCM kwamba wamehujumiwa na ushahidi wanao, sasa ni wakati mwafaka tunawaomba CCM na Tume yao ZEC ( Jecha) watowe vielezo vyao hadharani, kwenye jumuia za kitaifa na kimataifa pia kwenye magazeti wachapishe toleo maalum, ili kila mmoja wetu apate kujiridhisha juu ya ukweli wa suala hili. Pia tunamuomba Nd. Jecha atowe vielelezo vyake kwa yale mambo mengine ambayo hakuyataja ili tupate kumuamini, sio asubuhi ajifungie Mazizini usiku akalale Kiongwe Bumbwini, huku akijiandaa kutowa video nyengine ya kutangaza tarehe ya uchaguzi.

CCM na ZEC (Jecha) Mtakapo shindwa kutowa ushahidi wenu kwa uwazi itakuwa ni dhahiri kwamba ni waongo na mlikula njama ya kupindua maamuzi ya waliowengi kwa maslahi yenu binafsi.

Tunawaomba CCM mtuonyeshe ushahidi wenu kama mlivyo ahidi kupitia Waride Bakar Jabu ili dunia iwaunge mkono,kama hamna ushahidi msitafute sababu ya kumwaga damu kaeni kimya.

Mwisho nawaomba CCM na ZEC (Jecha) watafakari kwa makini kabla hawaja chukuwa maamuzi mabaya yatakayo pelekea machafuko, uhasama na umwagikaji damu usiokuwa wa lazima.

kauli_ya_jecha

GAZETI_LA_SERIKALI

Share: