Makala/Tahariri

KUHUSU ZIARA YA DR. SHEIN NCHINI DJIBOUTI

*THE CIVIC UNITED FRONT – CUF CHAMA CHA WANANCHI.*

*KUHUSU ZIARA YA DR. SHEIN NCHINI DJIBOUTI .*

*Imetolewa 12 May 2017.*

Djibouti ni nchi iliyo pembeni mwa Africa, Kusini mwa Red Sea ambapo Kusini mwa nchi hiyo imepakana na Eritrea, Magharibi imepakana na Ethiopia na Mashariki ya Kusini imepakana na Somalia.

Djibouti ni nchi yenye eneo la kilomita square 23, 200 na jumla ya watu 846,687 ambao wanatokana na makundi mawili makubwa, moja likiwa ni kundi la Somali lenye asilimia 60% ya wakaazi na jengine ni Afar lenye asilimia 35% ya wakaazi na asilimia 5% ni makundi mengine madogo. Idadi hii ya Wakaazi ni ndogo ukilinganisha na Zanzibar. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2002 Zanzibar ina watu wapatao 984,625 ambao 622,459 wanaishi Unguja na 362,166 wanaishi Pemba. Watu wa Djibouti ni Waislamu ambapo kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2013 asilimia 94% ya wakaazi wa Djibouti ni Waislamu.

Djibouti ilipata uhuru wake kutoka mikononi mwa ukoloni wa Ufaransa mnamo June 27 mwaka 1977 na ilitambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa kama nchi huru September 20/1977 ambapo kabla ya hapo Djibouti ilikua ni Koloni la Ufaransa. Katika hali hiyo Hassan Gouled Aptidon ndie aliekua raisi wa mwanzo wa nchi hiyo kabla ya huyu aliepo sasa ambaye ni Ismail Omar Guelleh. Hii ni sawa na kusema kua Zanzibar ni nchi iliyotambuliwa mwanzo zaidi na Umoja wa Mataifa kama nchi huru kuliko Djibouti ambayo Dr. Shein anawapotosha Wazanzibari ili ionekane ziara yake hiyo ni ziara kubwa ambayo haijawahi kutokea.

Djibouti ni nchi ambayo hali ya hewa yake ni ya joto (vuguvugu) na uchumi wake unategemea zaidi sekta ya huduma za bidhaa (Uchumi wa huduma -Service Sector Economy).

Kwa upande wa afya Djibouti inahudumia watu 100,000 kwa madaktari 18 kwa siku ambapo pia watoto wanaozaliwa wa kike na wa kiume kwa siku ni sawa na asilimia 63.2% na kati ya hao vifo vya watoto wadogo ni sawa na asilimia 2.35% kwa kila mwanamke. Pamoja na asilimia 94% ya Wakaazi wa Djibouti kua ni Waislamu asilimia 93.1% ya Wanawake wa nchi hiyo wamekwishatahiriwa (Femal Circumcision ).

Mpaka kufikia 2011 Djibouti ni nchi ambayo ina Majeshi wapatao 170,386 wa kiume na 221, 411 wa kike wenye umri wa kuanzia miaka 16 mpaka 49.

Djibouti ina vyama vya siasa 11 vinavyojulikana kama People’s Rally for Progress (PRP), Front for Restoration of Unity and Democracy (FRUD), Social Democratic People’s Party (SDPP), Union of Reform Partisans (URP), Union for National Salvation (UNS), Centre Democrate Unifie Djiboutien (CDU), National Democratic Party (PND), Republican Alliance for Democracy (ARD), Movement for Democratic Renewal and Development (MRD), Djibouti Party for Development (PDD) na Djibouti Union for Democracy and Justice (UDJ).

*TUTANUFAIKA NINI NA ZIARA YA DR. SHEIN NCHINI HUMO?*

Viwanda vya Samaki alivyoahidi Dr. Shein kua vitaanzishwa Zanzibar kupitia makubaliano yake na Serikali ya Djibouti inawezekana wazi kua huenda makubaliano hayo ni hewa hasa kwa kuzingatia kua Djibouti yenyewe uchumi wake na mapato ya Serikali yake asilimia 79% yanategemea zaidi huduma za bidhaa, asilimia 17.3% yanategemea Viwanda na asilimia 3% ya mapato yote ya Serikali kwa mujibu wa ripoti yake ya 2013 yanategemea kilimo.

Hii ni sawa na kusema kua asilimia hiyo17.3% ni asilimia ndogo sana kuliko ile ambayo nchi hiyo inaitegemea ambayo ni 79% ya huduma za bidhaa. Hii pia ni sawa na kusema kua Viwanda eidha sio kipaumbele cha Djibouti katika pato lake la Serikali au Djibouti haina mikakati na uwezo wa kutosha katika kuekeza kwenye Viwanda tofauti na Dr. Shein anavyowadanganya Wazanzibari.

Pia Djibouti ni nchi ambayo inaingiza asilimia ndogo sana ya Watalii nchini humo ambapo kuanzia mwaka1995 mpaka kufikia mwaka 2013 imeingiza watalii wasiozidi 63,000 kwa mwaka. Idadi hii ni ndogo ukilinganisha na Zanzibar ambapo kufikia mwaka 2005 Zanzibar iliingiza Watalii wasiopungua 100, 000 kwa mwaka.

Kwa upande wa Siasa, Djibouti ni nchi ambayo ina historia ya Vita vya wenyewe kwa wenyewe (Civil War) vya muda mrefu tangia miaka ya 1990s mpaka kufikia mwaka 2001 ambapo June 7 mwaka 2000 Chama cha Front for the Unity and Democracy (FRUD) kilitia saini Makubaliano ya Amani (A peace treaty) na Serikali ya Djibouti.

Hata hivyo Djibouti haikubaki salama hasa ukizingatia kua nchi hiyo ni nchi inayoongozwa na Chama kimoja (One party dominated state )kinachojulikana kwa jina la People’s Rally for Progress (RPP) ambacho kimeshikilia Madaraka tangia kuasisiwa kwake mwaka 1979.

Uchaguzi wa mwisho wa nchi hiyo ulifanyika tarehe 22 February 2013 na kusababisha Bwana Ismail Omar Guelleh kubaki Madarakani licha ya Wapinzani kupinga jambo hilo.

Guelleh anasifika kwa udikteta na kwa kuwanyima uhuru Wapinzani wake na Vyombo vya Habari nchini humo ambapo katika moja ya tukio linalokumbukwa nchini humo ni lile la Chama kikuu cha Upinzani nchini humo kuususia Uchaguzi wa 2005 kufuatia Serikali ya Djibouti kuvinyima uhuru Vyombo vya Habari na kuwakandamiza Wapinzani.

Pamoja na Chama hicho kususia uchaguzi huo, Guelleh aliapishwa tarehe 8 April 2005 kuiongoza tena kwa kipindi chake cha miaka 6 ya pili huku akijichukulia asilimia 100% ya ushindi katika asilimia 78.9% ya kura zilizopigwa.

Mwaka 2011 Wakaazi wa Djibouti waliandamana kupinga Serikali hiyo iliyodumu kwa muda mrefu ambapo Guelleh alilazimisha kugombea tena kwa kipindi cha tatu mwaka huo na kujichukulia ushindi wa asilimia 80.63% ya asilimia 75% ya kura zilizopigwa. Pamoja na Chama cha Upinzani kususia Uchaguzi huo kwa kile walichodai kua katiba ya Djibouti haimruhusu Guelleh kugombea tena kwa mara ya tatu (Irregularities )lakini Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Africa (Africa Union) walidai kua Uchaguzi huo ulikua wa huru na wa haki. Pia katika hali ya kushangaza zaidi Guelleh amesikika hivi karibuni akitangaza kua atagombea tena kwa kipindi cha nne katika Uchaguzi unaofata.

Kwa upande wa Haki za Binadamu, Djibouti inasemekana kua ni nchi ambayo haiheshimu uhuru wa Watu wake kwa mujibu wa ripoti ya ya Dunia ya mwaka 2011. Ripoti hiyo inaeleza kua watu wanakamatwa kinyume na sheria na hali za magereza (Prisoners )nchini humo ni mbaya sana. Mwaka 2011 Raisi wa Shirikisho la Haki za Binadamu nchini humo Bwana Jean Paul Noul Abdi alikamatwa kwasababu tu ya kuripoti tukio la Wapinzani kupinga Serikali ya Guelleh.

Kutokana na hali hiyo na mengine mengi yanayohusu nchi hiyo halitokua jambo la kushangaza tukisema yafuatayo;

> Kua ziara ya Dr. Shein haitaleta tija kama Dr. Shein alivyowadhihaki Wazanzibari pale Uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume.

> Ziara hiyo haikua na lengo lolote zaidi ya Dr. Shein anaetawala bila ya ridhaa ya Wazanzibari kwenda kumtembelea Dikteta Guelleh na kubadilishana mawazo juu ya namna bora ya kuwahujumu Wapinzani.

> Dr. Shein anawadhihaki wasiojua kwasababu tu ya kutaka kuhalalisha uwepo wake ambao umetokana na uharamu alioufanya yeye na Jecha Salim Jecha.

> Dr. Shein anataka aonekane kua anafanya kazi kama raisi ndani ya mipaka ya Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania jambo ambalo sio kweli. Mara zote alizosafiri kwenda nchi za Ulaya Dr. Shein hajapatapo kuskika akisema kua amekubaliana na nchi hizo kushirikiana katika sekta mbali mbali za maendeleo isipokua pale anapokwenda katika nchi za Africa ambazo nyingi zinaongozwa na Madikteta.

> Wazanzibari wasishtushwe na ziara hizo. Kioo bado kinamdanganya Dr. Shein na CCM wenzake na pamoja na kufanya kila wanalofanya kuifuta aibu na kipigo walichokipata kutoka kwa Wananchi wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi CUF October 2015 bado wanajikuta aibu na kipigo hicho kipo pale pale.

> CUF Chama cha Wananchi kitaendelea kudai haki ya Wazanzibari na kitaendelea kuwaelimisha Wananchi na kuwatolea ufafanuzi wa mambo mbali mbali yanayoendelea kufanywa na Serikali haramu ya Dr. Shein na genge lake ili kuwatoa wasi wasi na kuwajuvya mambo muhimu kwa mustakbali wa nchi yetu.

*HAKI SAWA KWA WOTE*

Imetolewa na;
Hijja Hassan Hijja
Msemaji wa Sekta ya BLMU.

FB

Share: