Makala/Tahariri

MAALIM SEIF KAMA HUJAWAJUA CCM, SUBIRI USHAHIDI WA ‘KINYAMWEZI’

Na: Mwandishi wetu

Katika visa vya kiutani vye kukirihi kidogo, kile cha mnyamwezi aliyesubiri ushahidi kamili ni mashuhuri zaidi katika jamii za hapa kwetu visiwani. Katika kisa hicho yasemwa kulikuwa na mnyamwezi katika mabanda ya kulalia wachuma karafuu huko Pemba, sijui Taifu au makuwe, sina uhakika sana kwa sasa! Umri.

Siku moja, usiku, wakati mnyamwezi amelala alishtushwa na hisia za kuguswa kunakoleta shaka kwa mwanamme. Shaka ambayo wakati kama huu wa kuadhimisha sherehe za mapinduzi, si vibaya nikimnukuu Sheikh Abeid Karume pale aliposema; ‘Mwanamme ni yule ambaye hakubali kuchezewa na mwanamme mwenziwe hata kwa dakika moja!’

Pamoja na kuwa mnyamwezi huyu alikuwa mwanamme, alivyojiita, kwa maoni ya Sheikh Karume, mnyamwezi huyu hakutimia uume wake. Hakutimia kwa sababu kila alipohisi kuguswa na mwanamme mwenzake, alinyamaza kimya kwa kisingizio cha kutaka apate ushahidi kamili ndipo achukuwe hatua zinazofaa! Kwa bahati ushahidi kamili aliupata lakini aibu ikabakia kwake hadi leo! Ndio ikasemwa kuwa kuna ushahidi wa kinyamwezi pale ambapo mtu husubiri hadi adhurike au aharibikiwe ndipo sasa achukuwe hatua.

Nimeanza ukurasa wangu huu namna hii kutokana na tukio linalokuja baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, ambapo bila kutafuna maneno, maalim Seif Sharif Hamad, wa CUF aliibuka kidedea na kumshinda vibaya vibaya mgombea wa CCM, HRH; the eternal Sultan and the last King of Zanzibar Island, Dr. Ali Mohammed Shein.

Mara zote tumekuwa tukimlaumu maalim kwa kushindwa kuzitambua na kuzifania kazi mbinu za CCM katika chaguzi ambazo miaka yote hufanyiwa hujuma na dhuluma. Kawaida ya Binadamu , anapodhulumiwa kwa miaka isiyopungua 20 na mtu huyo huyo, basi huwa tayari ameshajifunza vya kutosha juu ya njama za mtu anayemdhulumu. Na hivyo ndivyo alivyofanya maalim mara hii.

Tafauti na chaguzi zilizopita, mara hii maalim alikuwa na timu ya ushindi kwa maana ya timu ya ukweli kikweli kweli. Haikuwa timu ya wale mawakala njaa walio wakihongwa elfu tano wakaachia CCM waibe watakavyo kura na visanduku vyake. Mara hii ilikuwa roho kwa roho kweli. Zoezi la kura likapita salama na matokea halali yakakusanywa kwa ujasiri mkubwa na yakafika mtendeni salama.
Tafauti na chaguzi zilizopita, ambapo maalim akikaa kwake mtoni akisubiri atangazwe, mara hii aliiamua kujitangaza mwenyewe na kuwafanya CCM waghumiwe na wakose la kufanya kwa muda. Kitendo hiki nacho kwa tunavyowajua CCM kilikuwa kitendo muafaka alichokifanya maalim lakini baada ya tukio hili, maalim akaanza kuwasahau CCM na kaida zao.

Licha ya kuwa anawafahamu kwa miaka 20 nafikiri naye maalim alikuwa akisubiri ushahidi wa kinyamwezi kuthibitisha kuwa CCM sio binadamu wazuri kabisa. Kwani, baada ya maalim kujitangaza alikuwa ahamasishe watu waingie mitaani kwa gharama yeyote bila kujali vifaru wala jeshi akiamini kuwa nguvu ya wananchi ni kubwa zaidi kuliko ya jeshi. Hilo hakufanya baada ya kujitangaza.
Baada ya CCM kuona kuwa kasi ya maalim imekatika, wakafuta uchaguzi. Kisha wakakaa miezi mitatu wakipima nguvu ya maalim Seif na utayari wake. Wakauona. Ndipo walipoanza kumuita Ikulu na kumfanyia ujanja wa kumzunguka CCM watupu akibaki CUF peke yake huku wakimfunga mdomo asiseme kinachozungumzwa huko mpaka sisi wafuasi wake tukate tamaa.

Kwa wenye akili timamu walijua wazi kuwa, hakuna jema katika mazungumzo na CCM hata wangesimamiwa na Mtume. Wangeharibu tu. Lakini kwa kuwa maalim ni mtu wa kutaka ushahid kamili, alikubali akaitwa vikao nane huku akituacha na hofu na matumaini yetu yakififia.

Wakati matumaini yetu yakififia na nguvu ya ushindi ikipotea, CCM kupitia makada wao kama Balozi Mkaazi, Waride na Vuai, wakisambaza majungu ya kuwa hawajali kisemwacho ikulu. Uchaguzi upo kama kawaida.

Kauli hizi hazikuwa na nia njema lakini kwa kuwa maalim Seif licha ya kuwajua vyema CCM haamiini hadi apate ushahidi kamili, akanyamaza. Miezi miwili ikapita na CCM ikaweza kujizoazoa kutoka chini ilikokuwa imelala kwa kipigo kikali na kuamka na nguvu ya ajabu huku wana CUF wakiwa usingizini.
Vikao vinane vimekwisha, na hakuna lililokuwa kwa matarajio ya wananchi na maalim Seif. CCM imemuweka tena madarakani Dr. Shein na jeuri tele. Maalim kaamka tena jana lakini kaamka karamu ishaliwa. Zimebaki story! Uchaguzi unarudiwa kama kawaida na CUF haitashiriki.

Ningekuwa mimi ni maalim Seif, ningefanya yafuatayo bila kujali ya watu. Kwanza, baada ya kujitangaza ushindi tu ningewataka wafuasi wangu waingie barabarani kwa kauli moja tu, kushangilia ushindi. Na ikitokezea wakipigwa na Askari basi watumie uwezo wao dhaifu kuwapiga waliowapiga mpaka kieleweke.
Pili, baada ya uchaguzi kufutwa, ningeendelea kuwaongoza wananchi kushangilia nikiwa mstari wa mbele nchi nzima na kuzijaza barabara kuu zote za Unguja na Pemba kwa idadi kubwa ya watu ambao wamejitolea muhanga kufa au kupona kwa ajili ya kuikomboa nchi hii. Na kwa kauli hii nashika maneno ya Mansuri kuwa hatusubiri watoe, ‘tutang’an’amua’ kwa mikono yetu mara hii. Hili ndilo ningefanya.

Najua kuna watu wanajifanya na imani ya dini watasema watu watakufa bure. Ningepuuza hoja hii kwa sababu watu wa Zanzibar tayari ni maiti kwa hivyo hakuna hasara hata wakifa kuigomboa nchi yao ambao haitatoka kwa ‘vikaratasi’ vya kura. Pia nawaaminisha kuwa ingawa mnaona CCM ina jeshi, nguvu ya wananchi ni kubwa kuliko jeshi na silala zake. Hili liko wazi na ningelifanya. Potelea bondeni.

Tatu, hivi sasa, baada ya mazungumzo kushindikana, pia ningehamasihwa wananchi wote kufanya kila aina ya uasi na maandamano kila kona name nikiwa mstari wa mbele kudai haki ya nchi hii. Nafanya hivi kwa kuwa sasa hakuna njia nyengine ya amani ya kuigomboa nchi hii zaidi ya mapigano na mapambano ya watakavyo twataka!
Kwa bahati mbaya, maalim hatafanya haya na Mfalme Shein atabaki kuwa madarakani huku wakitufanya sisi waumini wa maalim Seif tukiamini kuwa yeye maalim ni BWEGE kama alivyosema Balozi mkazi wa Tanganyika. Ni bwege kwa sababu licha ya kuvitambua vitimbi vya CCM siku zote anabaki akisubiri ushahidi kamili tu. Ushahidi wa kinyamwezi, uliojaa aibu na kushindwa!
Maalim BADILIKA! Umma unao, unaogopa dola kwa nini?

Tagsslider
Share: