Maoni

VITUKO VYA MWEZI WA MTUKUFU WA RAMADHAN

Shukrani kwa wote waliojaaliwa kuufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan na kujaaliwa kuumaliza kwa afya na salama
Mimi si mtaalamu wa mambo ya dini ya Kislam lakini kidogo tu nina elimu ya chini ya mambo ya dini ya Kislam kwa sababu ni muumin wa dini ya Kislam
Ramadhan ndio inakwisha na waliojaaliwa wameona neema na barka zake na pia wameona vituko vilivyojitokeza kwenye mwezi huu
Baadhi ya vituko nilivyoviona na kunishangaza ni hichi cha Benki kufutarisha Benki ni kitengo cha fedha ambacho mapato yake mengi yanatokana na riba kwa mujib ninavyofahamu leo Benki inafutarisha na Masheikh wanaiombea dua wanawalisha watu au kuwafutarisha kwa faida ya riba jee jamani hii inakubalika?Vituko na viroja vilikuwa vingi mwezi huu lakini nawaomba wenye elimu ya dini watueleze huu uhalali wa Mabenki kufutarisha
Inawezakana elimu yangu ya dini ni finyu kwa hivyo kama nimekosea naomba samahani lakini ningependelea nielimishwe zaidi juu ya hili
Nawatakia Sikukuu Njema na ya Furaha ya Eid

Share: