MaadiliMakala/Tahariri

Masuali na Majibu na Sheikh Shaaban Al-Battashy

📘SWALI LA 1108 📘

✍Ninamchumba nilikuwa nachat nae, na akanimbia anataka kunioa, nikamuuliza huna mtu yoyote au hujaowa

akaniambia kuwa hajaoa. nami nikawa naendelea kuchat naye, siku moja akajitokeza mkewe na kuona sms zetu mimi na yeye, mke alikasirika sana nakudai talaka.
Nini hukmu yake

📘 JAWABU 📘


Ndugu zangu :
Posa ni ” Ahadi ya kuoana – kwa kupitia walii wa mwanamke – baina ya mwanaume na mwanamke ambao wanafaa kuoana kisheria ”


Ni makosa makubwa sana mwanaume na mwanamke kuposana wao kwa wao wawili bila ya kupitia walii wake.

>>> Na wakikaa mwanaume na mwanamke peke yao faragha basi wa tatu wao ni shetani katika kuwapotosha.

>>> Amma kikao cha kheri ni kile ambacho kinafanyika kwa mujibu wa sheria za ALLAAH S.W.

>>> Na lazima wakumbuke hao wanao chat na waume za watu, au wake za watu, katika njia ya faragha na siri kwa lengo la kufanya maovu au kuweka mahusiano ya ki mapenzi baina yao , wajue kuwa ALLAAH S.W anawaona mambo yao yote.

>>> Amesema ALLAAHU S.W :
(أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ مَا يَكُونُ مِنْ نَجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِنْ ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا ۖ ثُمَّ يُنَبِّئُهُمْ بِمَا عَمِلُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ إِنَّ اللَّهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ)
[Surat Al-Mujadala 7]

>>> Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu anajua vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi? Hauwi mnong’ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wane wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeye yu pamoja nao popote pale walipo. Kisha Siku ya Kiyama atawaambia waliyo yatenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

>>> Na dhambi inazidi kuwa kubwa zaidi ikiwa limefanyika hilo baina ya mtu na mke wa mtu au mume wa mtu.

>>> Na likisababisha Talaka baina ya mume na mke basi dhambi inazidi kuongezeka ubaya zaidi na zaidi, na siku ya qiyaama watalipwa na mola wao kila mmoja kwa alichokifanya.

>>> Yanayo akiwa kwa sasa ni haya yafuatayo :

1. Watubie kwa ALLAAH S.W wote wawili waliokuwa wakichat.

2. Wakate mawasiliani baina yao kabisa, na hiyo ni moja katika masharti ya toba sahihi.

3. Mume ajilazimishe kumfanyia mkewe wema zaidi kuliko alivyokuwa mwanzo, huenda kwa Taufiiqi ya ALLAAH S.W wema huo ukafuta makosa yaliyotangulia.

4. Pia mume afanye toba maalumu ya kosa la kusema uongo kuwa ” Hana mke ” wakati mke anae.

5. Na ikiwa mtu ataulizwa kama ana mke au hana, yeye akasema kuwa : ” Hana ” au amemuacha ” katika Kauli ya maulamaa wengi ni kuwa atakuwa ameachika mkewe kweli.

>>> NAMUOMBA ALLAAH S.W AWAHIFADHI VIJANA KUTOKANA NA SHARI ZA MATAMANIO YA HARAMU.

📘ALLAAHU AALAMU.

📘 U / SHAABAN ALBATTAASHY
👉Usichanganye haki na batili.

SHAABAN BIN SAALIM BIN HAMOUD AL BATAASHY
ZANZIBAR MAAHAD ISTIQAAMA. 2000-2003 AD.
CHUO KIKUU CHA NIZWA – OMAN – UALIMU NA UTAFITI WA KINALEZI YA KIISILAMU NA IDARA. (MIAKA MINNE)
MEENYEKITI – CHAIR MAN WA DAAWA COMETEE KUANZIA 2012.
MMOJA KATIKA MEMBER WA MAHKAMA YA KADHI MKUU ZANZIBAR.

Tagsslider
Share: