Makala/Tahariri

muungano wa ulaya

Gazeti la Serikali la DAILY NEWS (toleo la jana November 21, 2012, kwenye ukurasa wa 15) limechapisha makala yanayozungumzia hisia za Waingereza kuhusiana na Muungano wa Ulaya yaani European Union (EU) zinavyozidi kujielekeza katika kuuona uanachama wake katika Muungano huo hauna maslahi tena na nchi yao. Makala hayo yanasema utafiti huria uliofanywa mwezi Agosti mwaka huu umeonesha asilimia 61 ya wananchi wa Uingereza wanataka nchi yao ijitoe kutoka EU huku asilimia 39 wakitaka ibakie katika Muungano huo wa Ulaya. Sababu kubwa zinazotajwa kupelekea mabadiliko hayo ya fikra miongoni mwa wananchi wa Uingereza ni kuuona Muungano huo ni mzigo kiuchumi na hauongezi tija yoyote katika kuinua uchumi wa Uingereza. Wafanyabiashara nao wanasema urasimu mwingi wa sheria za EU unakwaza maendeleo ya biashara. Katika makala hayo, panasemwa kuwa kinachoweza kuzuia hisia za kujitoa EU kwa Uingereza ni iwapo madai ya nchi hiyo ya kutaka MABADILIKO yatazingatiwa. Mafunzo makubwa ninayoyaona hapa ni kwamba kumbe kinachotazamwa siku zote katika miungano ya nchi ni maslahi gani yanapatikana katika huko kuungana. Ndiyo maana Wazanzibari nao wakasema mfumo huu wa sasa hauna maslahi na Zanzibar na sasa wanataka mfumo mpya wa Muungano wa Mkataba ambao utakuwa wa heshima, wa haki na wenye usawa kwa nchi zote wanachama huku kila nchi ikiwa na mamlaka kamili kitaifa na kimataifa.

Kwa faida yenu, nanukuu sehemu ya makala hayo ambayo kwa bahati nzuri hata gazeti la Serikali limeona elimu iliyomo kiasi cha kuamua kuyachapisha:

“EUROPEAN UNION EXIT IS NO LONGER TABOO TOPIC IN BRITAIN

EUROSCEPTICISM has been exacerbated by the eurozone crisis and a British exit from the European Union is now being openly discussed – unless London’s call for reforms are taken seriously.

Britain’s ambivalence to the European project can be explained by a lingering conviction that the EU remains essentially a common market to facilitate trade, says Paul Whitely, professor of politics at Essex University.

“Britain became a member because there were economic advantages. It was very much focused on trade,” he told AFP.

It is perhaps to coincidence then that British support for EU membership has dropped sharply in the last five years as the economic crisis has taken hold, Whitely says.

A regular opinion poll that he organises found in August that 61 percent of Britons wanted to leave the EU compared to just 39 percent who wanted to stay in.

Philip Whyte, from the pro-EU think tank Centre for European Reform, agrees that the British “never really signed up to the political dimension of the EU, the stuff about developing the foreign policy dimension or the single currency”.

He traces a key reason for the growth in euroscepticism to the enlargement of the bloc towards eastern and central Europe in 2004.

After an estimated one million new EU passport holders flooded into Britain in the space of few years, “EU membership was associated with the loss of control at the UK borders,” said Whyte.

Another reason was that “the EU has been increasingly seen by the business community as the source of all sorts of unnecessary regulations”.

Hivi ndivyo hali ilivyo na hivi ndivyo wenzetu wanavyotafakari na kuchambua kwa hoja mambo yanayohusu mustakbali wao. Na sisi tunapaswa tuzungumze na kuchambua hadi tupate ufumbuzi kwa njia za amani, za kiungwana na kistaarabu, na kwa kutumia hoja. Hapana shaka yoyote tutafanikiwa kufikia ufumbuzi wa heshima, wa haki na wenye kuzingatia usawa. Hayo ndiyo pia mawazo ya watu waungwana na wanaojiheshimu na kuheshimika kama Jaji Mark Bomani.

Tagsslider
Share: