MaadiliMakala/Tahariri

Nani walii wa mtoto wa nje ya ndoa? Jibu na Sheikh Shaaban

📘SWALI LA 1087 📘
Nani walii wa mtoto wa nje ya ndoa?…au pia wazee wake wameoana lakini ni baada ya kuzaa kabla ya ndoa nani anasimama kuwa walii….baba yake inafaa na kama wazee wao wamemzaa bila ndoa na hadi sasa wazee wake hawajaona…..nani walii haswa wa mtoto wa nje ya ndoa?
🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷

📘 JAWABU 📘

➡ Ndoa ni mafungamano sahihi na masafi kati ya mume na mke katika misingi mikuu ya sheria za kiisilaamu.

➡ Na kutokana na umuhimu wa mafungamano hayo, Uisilamu umeweka nguzo na masharti katika ndoa, ili kuhakikisha kufanikiwa maslahi na kuondoa maharibiko .

➡ Walii ni moja katika nguzo kuu za ndoa, na ni sharti katika kusihi ndoa hiyo, na hii ndio Kauli sahihi ya jamhuri ya maulamaa wengi.

➡ Amesema ALLAAHU S.W :
(وَمَنْ لَمْ يَسْتَطِعْ مِنْكُمْ طَوْلًا أَنْ يَنْكِحَ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ فَمِنْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ مِنْ فَتَيَاتِكُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ۚ وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِكُمْ ۚ بَعْضُكُمْ مِنْ بَعْضٍ ۚ فَانْكِحُوهُنَّ بِإِذْنِ أَهْلِهِنَّ وَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ مُحْصَنَاتٍ غَيْرَ مُسَافِحَاتٍ وَلَا مُتَّخِذَاتِ أَخْدَانٍ ۚ

[Surat An-Nisa 25]

Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake wa kiungwana Waumini, na aoe katika vijakazi Waumini iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa imani yenu. Nyinyi mmetokana wenyewe kwa wenyewe. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao, na wapeni mahari yao kama ada, wawe wanawake wema, si makahaba wala si mahawara.

➡ Hapo ameamrisha ALLAAH S.W kuwa waozeshwe kwa idhini ya watu wao miongoni mwa mawalii, na si ndoa za wahuni wenye ukahaba.

➡ Na walii hawezi kuwa ila katika upande wa ubabani tu, kama vile : vile baba wa mwanamke, au kaka zake wa upande wa baba na kadhalika. …

➡ Na hawa wote ni lazima wawe ni katika wenye nasabu na mke huyo nasabu za asili, si kutokana na natija ya zinaa.

➡ Baba ambae ndie mtoto wa zinaa anatokana nae yeye, hana haki kisheria kuwa yeye ni walii wa mtoto wa nje ya ndoa.

➡ Na mtoto huyo walii wake anakuwa ni kadhi wa kiisilaamu au ambae anatawalia mambo ya waisilamu na yeye mwenyewe ni muisilamu.

➡ Imepokewa kutoka kwa mtume s.a.w amesema :
” فالسلطانُ ولِيّ من لا وليّ لهُ”

الراوي: عائشة أم المؤمنين المحدث: يحيى بن معين – المصدر: السنن الصغير للبيهقي – الصفحة أو الرقم: 3/16
خلاصة حكم المحدث: صحيح

➡ Sultan ni walii wa asiekuwa na walii ”

➡ Ameipokea imaamu Yahyaa bin Maiin.

➡ Na ikiwa hakuna kadhi basi jamaa katika kundi la waisilamu wa mji watatoa hukmu na kuidhinisha ndoa hiyo.

➡ Na hii ndio Kauli sahihi inayotegemewa katika jamhuri ya maulamaa.

➡ NAMUOMBA ALLAAH S.W ATUJAALIE WEMA KATIKA UHAI NA BAADA YA HAPO.

📘ALLAAHU AALAMU.

📘 U / SHAABAN ALBATTAASHY
🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷 🌷

” Kuhifadhi kizazi ni jambo la lazima katika makusudio ya dini “

Tagsslider
Share: