Makala/Tahariri

Pamela chuki na ujinga ndivyo vinavyokusumbua.

Na Rashid Abdallah

Handala, kijana aliyekadiriwa kuwa na miaka kumi, kwa mara ya kwanza alionekana mwaka 1969 huko Kuwait. Kila alipotembea Handala alifunga mikono yake nyuma, tangu alipofukuzwa katika ardhi yake, Handala hakuwa tena mrefu na umri wake ukabaki pale pale miaka kumi, hadi hapo atakapo rudi kwao ndio alitarajia umri wake uwendelee kuongezeka. Handala alivaa nguo chakavu bila ya viatu, ishara ya utii wake kwa masikini. Lakusikitisha ni kuwa Handala hakurudi tena nyumbni. Handala, kwanini aliyekumiliki walimuuwa?

“The Muhammad Art Exhibit and Contest was an anti-Muslim hate event; “The event in Garland wasn’t about freedom of speech; “It was about war with Islam; What the event’s organizers really want: it’s not free speech”. Hivyo ndivyo baadhi ya mitandao na magazeti yalivyoandika kuhusu, shindano la vibonzo vya kumchora Mtume Muhammad (saw).
Jina lake anaitwa Pamela Geller, ni mwana- Mama anayejitengenezea maadui kila jua likizama, anaongoza kundi lijiitalo “Stop Islamization of America” pia ni kiongozi wa shirika la the American Freedom Defense Initiative, ambalo ndio liliandaa shindano hilo . Ni shirika linalojihusisha na chuki dhidi ya Uislam na Waislam huko Marekani.

Jumapili iliyopita ndio, shindano la vibonzo vya kumkejeli mtume Muhammad (s.a.w.) lilifanyika, katika jimbo la Texas nchini Marekani. Pamela alikuwa ni mmoja wa waongozaji wa shindano hilo walilolipa jina la “The Muhammad Art Exhibit and Contest”.

Waandaaji wa shindano hilo wanadai kuwa ni uhuru wa kujieleza, chapisho la VOX kupitia mtandao, limeandika kuwa; “this was not principally a free speech event; it was an anti-Muslim hate event”, halikuwa hasa tukio la uhuru wa kujieleza ila tukio la chuki dhidi ya Waislam.
VOX unaongeza kwa kusema kuwa, wazo la kundi la Pamela ni kuunga mkono “chuki na kubaguliwa kwa Waislamu”. Pia mtandao huo unasema kuwa “uhalali wa kuenea mawazo ya shirika lake, ni kueneza chuki, uharibifu na hatari”.

Shirika la Southern Poverty Law Center, linalotetea haki za raia na maslahi ya umma, limelielezea kundi la Pamela kuwa ni kundi la chuki, nalo shirika la The Anti-Defamation League shirika lisilo la serekali, limelitaja Shirika la Pamela kuwa ni kundi la chuki na kuelezea lengo lake kuwa ni; “Promoting a conspiratorial anti-Muslim agenda under the guise of fighting radical Islam” and seek[ing] to rouse public fears by consistently vilifying the Islamic faith and asserting the existence of an Islamic conspiracy to destroy ‘American’ values”.

Ukweli ni kwamba hakuna uhuru wowote ambao Pamela anautetea, yeye na watu wake wana chuki dhidi ya Uislam, na wameshindwa kuficha chuki zao wanadhihirisha wazi wazi kuwa mishipa yao ya damu imejaa chuki. Nikupe mifano michache ya kukuonesha kuwa hakuna uhuru wa kujieleza unaopiganiwa isipokuwa ni chuki tu.

Wakati Charlie Hebdo iliposhambuliwa, Shirika la Kijamii la Muslim Public Affairs Committee UK’s, waliuliza kupitia ukurasa wao wa facebook; Ikiwa shambulio katika ofisi za jarida la Charlie Hebdo ni kupinga uhuru wa kujieleza, kwanini Rubert Murdoch aliomba samahani kwa kibonzo cha mauaji ya Waislam kilichomhusu Waziri mkuu wa Israel?
Turudi nyuma, mwaka 2013 gazeti la Ynetnews kutoka Israel tarehere 18/1 lilichomoza na habari iliyokuwa na anuani; “Murdoch apologizes for Sunday Times’ Netanyahu cartoon”. Yaani, Murdon aomba samahani kwa kibonzo cha Netanyahu katika gazeti la Sunday Times.
Mardoch, huyu ni mfanyabiashara mkubwa na Mkurugenzi mtendaji wa Australia’s News Limited. Aliomba msamaha kwa niaba ya gazeti lake la Sunday Times kwa kibonzo kilichomuonesha Waziri Mkuu wa Israel akijenga ukuta kwa kutumia matofali pamoja na miili ya watu wa Palestina, huku damu zao zikionekana ndio mchanga na saruji wa kuunganishia tofali moja na jengine au tofali na mwili wa Mpalestina. Aliomba samahi kwa kibonzo chenye sura hiyo.

Kisa chengine ni hiki, “Mimi si Charlie! Mimi ni Sinet. Nilikuwa mfanyakazi wa Charlie kama mchora vibonzo. Mwaka 2009, nilitengeneza kibonzo kikimuonesha Mtoto wa Sarkozy akibadili dini na kuingia katika dini ya Kiyahudi (Judaism) ili apate pesa. Charlie wakanitaka niombe samahani na nikakataa. Charlie wakanifukuza kazi kwa kuikejeli dini ya Kiyahudi”.
Hicho ndicho kilichomkuta mchora vikatuni vya kisiasa Sinet, kwa miaka 20 akiwa na jarida la kila wiki la Charlie Hebdo. Kwa kumchora mtoto wa aliyekuwa raisi wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, aitwaye Jean, kuwa anataka kubadili dini kutoka Ukatoliki na kuingia Dini ya Kiyahudi kwa sababu ya mwanamke tajiri wa Kiyahudi.

Mhariri wa jarida hilo, Phillippe Val, alimtaka Sine kuomba msamaha lakini alikataa, na mwisho wake ulikuwa ni kufukuzwa kazi.
18 July, 2013 mtandao wa The Wall Street Journal, ulikuwa na habari inayosema; France Bans Planned Pro-Palestinian Rally in Paris, kisha mtandao huo ukaanza katika aya ya kwanza ya habari hiyo kwa kusema; Mamlaka ya Ufaransa imepiga marufuku makundi ya watu wanaounga mkono Palestina kufanya mikutano ya hadhara katika jiji la Paris siku ya Jumamosi.

Matukio hayo yote yanaonesha, kuutusi Uislam ni uhuru wa kutoa maoni lakini akitokea mtu akiutusi Uyahudi basi huyo atachukuliwa hatua, shirika litaomba radhi au mfanyakazi atafukuzwa kazi, kama si chuki dhidi ya Uislam hakukuwa na haja ya watu kuzuiwa kufanya mikutano, kama ni uhuru wa kutoa maoni hakukuwa na haja ya Sinet kufukuzwa kazi.

Saka la HB lilipokuwa likiendelea, mwandishi wa BBC, Tim Wilcox wakati akiwa Paris kufuatilia tukio lile, alizungumza na mama mmoja wa Kiisrael ambaye alikuwa akielezea hofu yake, na kusema kuwa Waisrael ndio wamekuwa wakilengwa sana sasa. Tim aliijibu hofu ya mama yule kwa kumwambia kuwa; Palestinians suffered hugely at Jewish hands as well”

Jawabu hii ya Tim, ilizusha lawama kubwa mno na akatakiwa aache kazi ya Uwandishi haraka na watu mbali mbali duniani, kwa kua maoni yake ni kuwa, Wapalestina wanateseka pia katika mikono ya Mayahudi. Kauli hii ilimpelekea Tim kuomba msamaha kupitia mtandao wake wa kijamii.
Kinachoonekana hapa ni chuki tu hakuna uhuru wa kutoa maoni ambao unapiganiwa, nafuu kuwa Pamela yeye ameshindwa kuzificha chuki zake na ameamua kuzionesha hadharani.

Nimalizie kisa hiki. Ni miongo miwili na miaka kadhaa, tangu mauaji ya Naji Salim al-Ali, mchora vibonzo maarufu aliyeuwawa Uingereza katika jiji la London nje ya Ofisi za gazeti la Kuwaiti lijuulikanalo kama Al Qabas.

Mtandao wa World Bulletin kutoka Uturuki (Turkey) mwanzoni mwa mwaka 2015 ilkuwa na habari iliyosomeka; 27 years since Handala cartoonist’s assassinatio, kisha ukaandika; Naji Salim al-Ali was shot by an Israeli Mossad agent on July 22, 1987. Maana yake ni kuwa Naji Salim al-Ali alipigwa risasi na wakala wa Shirika la Kijajusi la Israel (Mossad) July 22, mwaka 1987.

Handala ama kwa lugha ya kiarabu ni Handhwala, ni mhusika katika sanaa ya uchoraji vibonzo ya Naji Salim al-Ali. Handala ni kijana aliyekadiriwa kuwa na miaka kumi, kwa mara ya kwanza kibonzo hiki kilionekana katika karatasi za gazeti la Al-Siyasa huko Kuwait katika mji mkuu wa Qatar mwaka 1969 .
Kibonzo hiki kilikuwa na sifa wakati wa uchorwaji wake, alipotembea Hadala alifunga mikono yake nyuma, tangu alipofukuzwa katika ardhi yake ya Palestina Handala hakuwa tena mrefu na umri wake ukabaki pale pale miaka kumi, hadi hapo atakapo rudi kwao ndio alitarajia umri wake uwendelee kuongezeka. Kibonzo hiki pia kilizoeleka kwa kuvishwa uhusika wa kuvaa nguo chakavu bila ya viatu, ishara ya umasikini.

Naji Salim alimchora Handala siku zote kama mpinzani wa siasa za ukandamizaji, unyonyaji, ubabe, mauaji za Israel dhidi ya taifa la Wapalestina. Kama historia inavyotueleza maisha ya mmiliki wa Handala yalifika ukingoni kwa kupigwa risasi na wanaodaiwa kuwa mawakala wa Mossad, alipigwa katika uso na alikufa baada ya wiki tano katika Hospitali ya Charing Cross August 29, 1987 na kuzikwa katika makaburi ya Brookwood Islamic Cemetery nje ya London.
Yanayoandikwa kuhusu Judaism wanatafsiri kuwa ni kuidhalilisha dini hiyo lakini kwa dini nyegine ni uhuru wa kujieleza. Uhuru huu vipi munautambua kwa upande mmoja na upande mwengine unakuwa hautambuliki?

Kipi kilimfanya Sine afukuzwe kazi, kama HB wanazungumzia uhuru wa kujieleza? Kipi kilipelekea Mossad wamuue Naji Salim kama kweli kuna uhuru wa kujieleza? Wanao ivunjia heshima Israel wanaomba samahani kwa sababu ya vibonzo vyao, lakini vibonzo vinavyokashifu imani nyegine, vimekuwa ni uhuru wa kujieleza..

Kwa nchi za Ulaya ni marufuku kutumia nembo za Kinazi, lakini matusi kwa imani nyengine ni halali na ni haki yao kuyatoa.Dogo kuhusu Wayahudi linakuwa kubwa, uliza nini kilimkuta Anelka mchezaji wa mpira wa miguu raia wa Ufaransa kutuhumiwa kutoa ishara ya Kinazi wakati akishangilia goli.

Wakati Cahrlie Hebdo iliposhambuli, jumuiya ya Katoliki ya Marekani nayo ilikosoa kwa kusema kuwa Charlie Hebdo limekuwa likichochea mauaji kwa kuhujumu matukufu ya dini mbalimbali kwa kisingizio cha uhuru wa kuzungumza, pia jumuiya hiyo ikasema kuwa, Mhariri wa Charlie Hebdo, Stephane Charbonnier hakuelewa mchango alioutoa yeye mwenyewe katika kuchochea mauaji yake.

Charlie Hebdo ilishambuliwa lakini hata shindano la kumchora Mtume lilipofanyika siku ya Jumapili, nalo pia lilishambuliwa, lakini ukweli wa mambo utabaki kuwa, aliyeshambulia hata awe Muislamu,Mkristo, mujahidina,Yahudi,takfiri,gaidi,false flag,ametumwa, lakini dharau,chuki,kutojali,kebehi vimekuwa ndio mwanya,sababu na chanzo cha wao kubeba silaha na kushambulia.

Heshima ni jambo la msingi, matusi kwa dini nyengine ni chuki zilizopo lakini uhuru wa kujieleza ni kisingizio. Yasmina Khadra alipokuwa anahojiwa na Aljazeera katika kipindi cha Talk to Aljazeera, alisema ‘Usiukubali Uislam lakini uheshimu’.

Pamela na kundi lake anaonekana wazi kuwa amekosa heshima na Uislam, chuki na ujinga vinamsumbua, lakini siku zote vyovyote iwavyo mtu anatengeneza maadui wake kwa mikono yake ni kama afanyavyo Pamela.
Kila litokealo basi lina sababu ama chanzo wakati mwengine mauaji yanayofanyika huwa yamepaliliwa na chuki, chuki zako ndio huenda zikasababisha watu wakuandame.

Juzi Bill O’Reilly alipokuwa akihojiwa na Fox News kuhusu tukio la kushindana kumchora Mtume na maana ya uhuru wa kuzungumza, alisema kuwa; if they never have that event the Jihadists will never shown up.

Share: