MaadiliMakala/Tahariri

Suali na Jibu la leo kutoka kwa Sheikh Shaaban Al-Battashy

📘SWALI LA ” 1190″📘
Naomba nisaidie hili:

Mimi ni muislamu, pia ni mtumishi wa serikali, miongoni mwa kazi zangu ni kukagua nyama ( meat inspection) kwa usalama wa mlaji.

Hivyo kwa mazingira yanayo nizunguka kuna watumiaji wengi wa nguruwe, je ninavyokagua na kuwaruhusu kuwa ipo safi na Salama kwa kuliwa, mimi sipati dhambi kwa muumba wangu?
🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷

📘JAWABU 📘

➡ Namuomba Allaah atukinge na madhara makubwa kama haya na mfano wake.

➡ Kazi hiyo ni miongoni mwa kazi zinazo harakisha kupelekwa motoni ikiwa mfanyaji wake hakutubia kwa haraka na kuiacha.

➡ Jukumu la kuhalalisha na kuharamisha ni la Allaah sw peke yake, na pia mtume saw ana jukumu hilo amepewa na Allaah sw, lakini haharamishi wala kuhalaliasha ila kwa kupewa wahyi – elimu kutoka kwa Allaah sw mwenyewe.

➡ Kinyume na wao wawili basi hakuna mwenye ruhusa hiyo ila maulamaa wachamungu wenye ujuzi wa ndani katika dini, nao ili kutoa fatwa ya uhalali au uharamu wa kitu ni lazima wawe na matejeo Katika Qurani au sunna.

➡ Amesema ALLAAH SW:
(وَلَا تَقُولُوا لِمَا تَصِفُ أَلْسِنَتُكُمُ الْكَذِبَ هَٰذَا حَلَالٌ وَهَٰذَا حَرَامٌ لِتَفْتَرُوا عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ)
[Surat An-Nahl 116]

Wala msiseme uwongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hichi halali, na hichi haramu – mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu. Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa.

(مَتَاعٌ قَلِيلٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ)
[Surat An-Nahl 117]

Ni starehe ndogo, nao watapata adhabu chungu.

➡ Kutokana na Aya hiyo na ziko nyingine nyingi mfano wa hiyo, wewe na pia yotote yule Katika viumbe, hauna haki wala madaraka yoyote ya kuhalaliasha kilicho haramishwa na Allaah sw.

➡ Hata ikiwa kazi hiyo ni kazi uliyo ajiriwa serikalini, au kazi yako binafsi, hakuna haki yotote ya kuhalaliasha au kuthibitisha kufaa kutumia nyama ya nguruwe , eti kwa kudhani kuwa elimu na utaalamu Ndio vinaweza kugundua madhara au manufaa ya kitu.

➡ Kumbuka kuwa, kuruhusu kwako watu watumie nyama ya nguruwe kwa kuwa unadhani kuwa haina madhara, ni dhambi kubwa na hatari, na huenda ukawa umeshatoka katika uisilamu pengine, ikiwa utaona kuwa hukmu yako wewe ni sahihi au ni bora zaidi kuliko hukmu ya Allaah sw.

➡ Na juu ya hayo unakuwa wewe ni Sawa na hali zifuatazo :

1- Ni Sawa na kujiona kuwa wewe ni Mungu mwingine unaweka sheria zako mwenyewe.

2- Ni sawa na kuhalaliasha yaliyo haramishwa na Allaah sw.

➡ Tubu kwa Allaah sw, na kazi hiyo iache Haraka kabla mauti hayaja kufika, yakifika Mauti na wewe bado uko katika kazi hii basi ujilaumu nafsi yako mwenyewe.

➡ Hata kama hiyo ni kazi yako huko serikalini hakuna ruhusa kwa muislamu kufanya kazi inayo muudhi Allaah sw na kuvunja misingi ya Dini.

➡ Nakumbusha pia wale wakemia wote wanaoruhusu pombe kuwa inafaa na wala haina madhara kitaalamu, wakumbuke kuwa wao ujuzi wao haumfikii Muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo.

➡ Hukmu Yao ni sawa na hukmu ya suala la mwanzo, na kuingia katika ukafiri ni njia ya karibu Sana kwa kazi chafu kama hizo.

📘NAMUOMBA ALLAAH SW ATUNUSURU NA MADHAMBI NA KUKUFURU.

📘ALLAAHU AALAMU

📘SWALI KUTOKANA KWA MUULIZAJI KAWAIDA.

📘JAWABU KUTOKA KWA U / SHAABAN AL BATTAASHY
🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷

” Ukiwa huoni haya kwa mola wako basi fanya utakavyo “

Tagsslider
Share: