MatangazoVifo

TAARIFA YA MSIBA KUTOKA NAPOLI,ITALIA

KIDISHI MCHEZAJI WA ZAMANI BLACK FIGHTER HATUNAE TENA

JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MTANZANIA MAREHEMU MAULIDI HAMID ABDALLA MAARUFU KWA JINA LA KIDISHI.

Kidishi amefariki siku ya jumanne ya tarehe 7/01/2014 usiku . Marehemu amefariki katika hospitali ya COTUGNO mjini Napoli, baada ya kulazwa kwa muda wa wiki tatu.

Marehemu katika uhai wake amewahi kucheza mpitra timu ya Black Fighters na hata Timu ya taifa zote za Zanzibar katika miaka ya themanini.

Mipango ya mazishi inafanywa na tayari yameshafanyika mawasiliano na familia ya marehemu.

TUNAPENDA KUWATANGAZI WATANZANIA WOTE KUWA KUTAKUWA NA MKUTANO WA HARAMBEE YA KUCHANGIA MIPANGO YA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU NYUMBANI KWA MAZISHI , MKUTANO UTAFANYIKA PALEPALE ULIPOFANYIKA MKUTANO WA KWANZA WA MAREHEMU JUMA KIJUU.

MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA.. AMIN!

Share: