Habari-PichaMatangazoUjumbe maalum

Taarifa za Sala ya Eid Hounslow

Assalamu Alaykum
Madrasatunnur Educational Trust iliopo mji wa Hounslow inapenda kuwaarifu waislamu wote waishio mji huo na miji ilioizunguka mji huo kuwa Inshaallah tutasali Sala ya Eid el Fitr kwenye ukumbi wa Madrasatunnur uliopo kwenye estate ya Convent way Community Hall kuanzia saa Mbili za Asubuhi.

Sala hiyo itategemea na taarifa za kuandama kwa Mwezi, na Inshaallah tunategemea kutazama mwezi kwenye tarehe 17/08/12 na ikiwa utaonekana siku hiyo basi Eid itakuwa tarehe 18/08/2012 ikiwa hakuna Taarifa za kuonekana, vyenginevyo Inshaallah tutasali tarehe 19/08/2012.

Vile vile tunachukua nafasi hii kuwakumbusha waumini wote wasisahau kutoa zakatul fitr zao ili kuzitakasa Swaumu zetu.

Kwa Niaba ya Madrasatunnur Educational Trust tunawatakia Waislamu wote duniani Eid Njema.

Share: